Star Tv

Tanzania yachukua Uenyekiti wa Nchi 79 za OACPS na kuelezea kipaumbele chake wakati wa Uenyekiti wake.

Tanzania imesema itatumia kipindi chake cha uenyeketi wa nchi za Afrika,Caribbean na Pacific na Umoja wa nchi za Ulaya katika kusisitiza juu ya urejeshwaji wa rasilimali zilizoporwa katika nchi hizo nyakati za ukoloni,kuheshimu mamlaka ya nchi husika na urejeshwaji wa wahamiaji haramu kwa kuzingatia utu na haki za binadamu.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dr. Damas Ndumbaro ameyasema hayo wakati akishiriki mkutano wa dharura wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa jumuiya ya nchi za Afrika,Caribbean na Pacific (OACPS) ambapo Tanzania inapata heshima ya kukabidhiwa Uenyekiti wa Jumuiya hiyo kwa ngazi ya Balozi na Waziri katika nchi 79 za jumuiya hiyo.

Ameongeza kuwa mbali na masuala hayo pia Tanzania katika kipindi chake cha uenyekiti itatilia mkazo zaidi suala la mashirikiano ya kiuchumi ili kuziwezesha nchi zote za Jumuiya ya Afrika,Caribbean na Pacific kuingia katika uchumi wa kati ili kupunguza umasikini miongoni mwa wananchi wake jambo litakalosaidia kupunguza uhamiaji haramu na kupunguza uhalifu wa kimataifa miongoni mwa nchi hizo.

Aidha, amesema kuwa hoja nyingine ni kuhusu majadiliano yanayoendelea hivi sasa kati ya Nchi za Afrika,Caribbean na Pacific na Jumuiya ya Ulaya ya kupata mkataba mpya baada ya kumalizika kwa mkataba wa Kotonu uwe ni mkataba wenye manufaa kwa pande zote mbili utakaokuwa na msukumo katika suala la maendeleo.

 

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.