Star Tv

Takriban watu sita wameripotiwa kufariki baada ya bomu kulipuka katika mgahawa mmoja uliopo mji wa kusini wa Somalia wa Baidoa.

Watu wengine kadhaa wamejeruhiwa. Ndani ya mji mkuu wa Mogadishu maafisa wa polisi wanasema kwamba walimpiga risasi mlipuaji wa kujitoa muhanga alipokuwa akiendesha gari lake katika kituo kimoja cha kukagua magari nje ya Bandari ya Mogadishu.

Taakiban watu saba walijeruhiwa katika shambulio hilo, Kulingana na mwandishi wa BBC Somalia Rage Hassan wote waliofariki katika mgahawa walidaiwa kuwa raia waliokuwa wakila kifungua kinywa, wakati bomu hilo lilipolipuka.

Maafisa wa usalama wa Somalia walikuwepo katika eneo hilo lakini hawakujeruhiwa.

Katika shambulio hilo Polisi waliambia shirika la BBC kwamba mlipuaji huyo wa kujitolea muhanga aliekuwa akiendesha gari hilo alijaribu kushambulia kituo cha kukagua magari barabarani mbele ya bandari lakini maafisa wa polisi walifanikiwa kumpiga risasi na gari hilo likalipuka.

Maafisa wawili wa polisi na raia watano walijeruhiwa.

Milipuko ya mabomu pamoja na mashambulizi ya kigaidi yamekuwa kitu cha kawaida mjini Mogadishu.

Hata hivyo hakuna mtu aliyedai ama kundi lolote lililodai kwamba alihusika na shambulio hilo.

Lakini kundi linalohusiana na lile la al-Qaeda limekuwa likijaribu kuiangusha serikali inayoungwa mkono na Muungano wa Afrika na hivyobasi kutekeleza mashambulio kama hayo.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.