Star Tv

Mkuu wa shirika hilo, Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema virusi vinaweza kuathiri watu wengi zaidi kwa siku za usoni ikiwa serikali hazikuanza kutekeleza sera sahihi.

Hali bado inaweza kuwa mbaya zaidi wakati huu wa janga la Covid-19, Shirika la afya duniani (WHO) limetahadharisha, miezi sita ikiwa imepita tangu mlipuko wa ugonjwa huo kutokea.

Zaidi ya watu milioni 10 wamethibitishwa kuwa na maambukizi duniani tangu virusi hivyo vilipojitokeza nchini China mwishoni mwa mwaka jana, Huku idadi ya wagonjwa waliopoteza maisha sasa ni zaidi ya 500,000

Nusu ya idadi ya watu walioambukizwa duniani imekuwa Marekani na Ulaya, lakini idadi inaongezeka kwa kasi Amerika.

Virusi hivyo pia vinaathiri Kusini mwa Asia na Afrika, ambako hakutarajiwi ongezeko la juu mpaka mwishoni mwa mwezi Julai.

Kukiwa na wagonjwa milioni 10 sasa na vifo vya watu nusu milioni, mpaka pale matatizo yaliyogundulika yatakajulikana na WHO, ukosefu wa umoja wa kitaifa na kidunia na dunia iliyogawanyika hali inayosaidia kusambaa kwa virusi…bado hali itakuja kuwa mbaya zaidi,'' alisema.

Amezitaka serikali kufuata mifano ya Ujerumani, Korea Kusini na Japan, ambazo zimekuwa zikichukua hatua kudhibiti maambukizi kwa kutumia sera ikiwemo vipimo na ufuatiliaji.

Marekani imeripoti kuwa na watu milioni 2.5 walioathirika na vifo karibu 126,000 vilivyotokana na Covid-19 mpaka sasa- zaidi ya taifa jingine lolote.

Majimbo ya nchini Marekani katika wiki za hivi karibuni- hasa kusini yameripoti ongezeko la maambukizi mapya.

Ongezeko hilo limefanya maafisa wa Texas, Florida na majimbo mengine kuweka mazuio makali tena kwenye biashara.

Nchi ya pili iliyo na kiasi kikubwa cha maambukizi ni Brazil, iiwa na watu walioambukizwa milioni 1.3 na vifo zaidi ya watu 57,000.

Siku ya Jumatatu hali ya dharura ilitangazwa katika mji mkuu Brisilia, kutokana na ongezeko la maambukizi.

Latest News

TEMBO 170 KUPIGWA MNADA NAMIBIA.
03 Dec 2020 10:05 - Grace Melleor

Tembo 170 watapigwa mnada nchini Namibia kwa kile kilichobainishwa kuwa ni adha ya kuongezeka kwa ukame huku kukishuhudi [ ... ]

BOKO HARAM WAKIRI KUTEKELEZA MAUAJI YA WAKULIMA 78.
02 Dec 2020 08:42 - Grace Melleor

Wanamgambo wa kundi la Kiislamu la Boko Haram wametoa video mpya ambayo inasema wapiganaji wake wa Boko Haram ndio walio [ ... ]

BOBI WINE AAHIRISHA KAMPENI ZA URAIS.
02 Dec 2020 08:19 - Grace Melleor

Mgombea wa urais nchini Uganda Robert Kyagulanyi, anayefahamika zaidi kama Bobi Wine ameahirisha kampeni zake.

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.