Star Tv

Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania Abubakar Zubeir bin Ally kwa niaba ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), ametangaza kuwa mwaka huu hakutokuwa na ibada ya hijja.

Hii ni kutokana na kauli iliyotolewa wiki hii na serikali ya Saudi Arabia kutokana na janga la Corona.

Mufti Zuberi ameyasema hayo leo Juni 25, 2020 wakati akiongea na waandishi wa habari ambapo ameeleza kuwa janga la Corona ndio limesababisha na haitakuwa kwa Tanzania pekee tu bali kwa Dunia nzima isipokuwa waislam waliopo ndani ya Saudi Arabia.

Sheikh Zuberi ameeleza kuwa BAKWATA wameunga mkono maamuzi hayo ya Saudi Arabia lengo likiwa ni kuweka usalama kwa waumini na kuwakinga na Corona kwasababu ugonjwa huo ni wa kuambukiza.

Aidha, Mufti Zubeir amezitaka madrasa zote nchini kuanzia sasa kurejesha shughuli zote za madrasa nchini huku zikizingatia taratibu zote za kiafya kama inavyoshauriwa na wataalamu wa afya nchini.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.