Star Tv

Rais wa Marekani Donald Trump ameongeza muda wa kusitishwa kwa visa za bahati nasibu pamoja na zile za wafanyakazi wa kigeni hadi mwisho wa 2020.

Wafanyakazi wenye ujuzi mkubwa wa kiufundi na wafanyakazi wasio katika sekta ya kilimo na maafisa wakuu wa makampuni ndio wataathirika, Huku Ikulu ya Marekani ikisema kwamba hatua hiyo itabuni ajira kwa Wamarekani wasio na kazi kutokana na mlipunko wa corona.

Kwa upande wa wakosoaji wanasema kwamba Ikulu ya Whitehouse inatumia janga la corona ili kukaza sheria za uhamiaji.

Katika mkutano na vyombo vya habari utawala wa rais huyo umesema usitishwaji huo utakaoendelea hadi mwisho wa mwaka huu utawaathiri watu 525,000.

Watu hao ni pamoja na 170,000 waliozuiliwa na hatua ya kusitisha visa za bahati nasibu - ambazo zinawapatia raia wa kigeni makaazi ya kudumu nchini Marekani.

Ikulu ya Whitehouse kwa mara ya kwanza ilitangaza kwamba ilikuwa inasitisha visa hizo mwezi Aprili agizo ambalo lilitarajiwa kukamilika Jumatatu.

Hatahivyo raia wa Kigeni walio na visa kwa sasa hawataathirika kufuatia sheria hizo mpya zilizotangazwa siku ya Jumatatu.

Agizo hilo pia litawashirikisha wale walio na visa aina ya H-1B, ambazo nyingi hupewa wafanyikazi wa Kihindi ambao wana ujuzi wa kiufundi.

Aidha, wakosoaji wanasema kwamba visa kama hizo zimeruhusu kampuni za Teknolojia za Silicon Valley kutoa kazi kwa raia wa kigeni wanaolipwa mishahara midogo.

Agizo hilo litasitisha kwa muda Visa nyingi aina ya H-2B kwa wafanyakazi wa msimu wakiwemo wale walio katika sekta ya utalii, isipokuwa wale wa kilimo, viwanda vya chakula na watalaam wa afya.

Latest News

AJALI YAUA WATU WATANO MKOANI DODOMA, WAWILI WAJERUHIWA.
03 Jul 2020 10:12 - Grace Melleor

Kamanda wa Polisi mkoani Dodoma Gilles Muroto amethibitisha kutokea kwa ajali ya gari aina ya Noah ambayo ilikuwa ikitok [ ... ]

ZTTO NA WENZAKE 07 WATAKIWA KUREJEA TENA POLISI.
01 Jul 2020 14:30 - Grace Melleor

Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo , Zitto Kabwe na viongozi wengine saba wa Chama hicho wameripoti Kituo Kikuu cha Pol [ ... ]

HALI YA MAAMBUKIZI YA CORONA YAWEZA KUWA MBAYA ZAIDI.
30 Jun 2020 13:13 - Grace Melleor

Mkuu wa shirika hilo, Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema virusi vinaweza kuathiri watu wengi zaidi kwa siku za usoni iki [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.