Star Tv

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa mkuu wa mkoa ambaye alikuwa ni Mrisho Gambo.

Rais Magufuli ametengua uteuzi huo leo Juni 19,2020, ambapo mbali na Gambo kutenguliwa kuwa Mkuu wa Mkoa huo pia wapo viongozi wengine wametenguliwa uteuzi wao na ameteua viongozi wengine kushika nafasi zao.

Aliyeishika nafasi ya Mrisho Gambo ni Bw.Idd Kamanta ambaye ndiye atachukua nafasi ya mkuu huyo wa mkoa, Kabla ya uteuzi huo Bw.Kamanta alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Monduli ambapo nafasi yake ya ukuu wa wilaya itajazwa baadaye.

Rais ametengua uteuzi wa Mkuu wa Wilaya ya Arusha Bw.Gabriel Daqarro na amemteua Bw.Kenan Kihongosi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Kabla ya uteuzi huo Bw.Kihongosi alikuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Iringa.

Pia Rais ametengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Dkt.Maulid Madeni na amemteua Dkt.John Pima kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha, Ambapo kabla ya uteuzi huo Dkt.Pima alikuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua Mkoani Tabora.

Aidha, Rais Magufuli amemteua Bw.Jerry Mwanga kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua, Kabla ya Uteuzi huo Bw.Mwanga alikuwa Afisa katikaOfisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).

Wateuzi wote wanatakiwa kuwepo Ikulu ya jijini Dar es Salaam ifikapo Juni 23,2020 saa mbili asubuhi.

Latest News

AJALI YAUA WATU WATANO MKOANI DODOMA, WAWILI WAJERUHIWA.
03 Jul 2020 10:12 - Grace Melleor

Kamanda wa Polisi mkoani Dodoma Gilles Muroto amethibitisha kutokea kwa ajali ya gari aina ya Noah ambayo ilikuwa ikitok [ ... ]

ZTTO NA WENZAKE 07 WATAKIWA KUREJEA TENA POLISI.
01 Jul 2020 14:30 - Grace Melleor

Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo , Zitto Kabwe na viongozi wengine saba wa Chama hicho wameripoti Kituo Kikuu cha Pol [ ... ]

HALI YA MAAMBUKIZI YA CORONA YAWEZA KUWA MBAYA ZAIDI.
30 Jun 2020 13:13 - Grace Melleor

Mkuu wa shirika hilo, Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema virusi vinaweza kuathiri watu wengi zaidi kwa siku za usoni iki [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.