Star Tv

Rais Uhuru Kenyatta ameutaja ushindi wa Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa baada ya kushinda Djibouti katika duru ya pili ya uchaguzi Alhamisi ni ushindi uliotukuka kwa kuonyesha baraza la Afrika nalo linaweza ungana na mataifa mengine makubwa ulimwengu kushiriki mambo duniani.

Kenyatta ameuelezea ushindi huo kuwa ni kukua kwa wasifu wa nchi hiyo na ushawishi wake miongoni mwa mataifa kama hatua isiyoyumbishwa na lolote na kwamba ni mshirika muhimu wa maendeleo.

Pia amewashukuru washindani wake katika uchaguzi huo, nchi ya Djibouti kwa kuwa mpinzani muhimu na Umoja wa Afrika kwa idhinisho lao kama mpeperusha bendera wa bara la Afrika kwenye kinyang’anyiro hicho.

Rais huyo wa Kenya, amesema, nchi hiyo itajitahidi kadiri ya uwezo wake kuunganisha Afrika na kusimamia msimamo wa bara hili katika Baraza la Usalama kwa kuendeleza ajenda zake 10 kama zilivyoonyeshwa wakati wa kipindi cha kampeni.

Kenya imeshinda Kinyanganyiro hicho kati yake na Djibout, Ambapo waliingia katika duru ya pili baada ya matokeo ya duru ya kwanza kuonesha kwamba Kenya haijapata kura za kutosha kuiwezesha kushinda nafasi hiyo ya Umoja wa Mataifa moja kwa moja.

Huku nchi 191 zikipiga kura kati ya 193, Kenya ilipata kura 129 na kuipiku Djibouti kwa kura 62, Ambapo baada ya panda shuka zo joto la kisiasa, Kenya imeiangusha Djibouti na kunyakua kiti hicho katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UN).

Kenya sasa itakaa katika baraza hilo linalopitisha maazimio muhimu duniani kwa muhula wa miaka miwili, Baraza hilo ambalo lina wanachama 15, nchi tano, Ambapo China, Marekani, Ufaransa, Urusi na Uingereza ni wanachama wa kudumu.

Nchi 10 zilizosalia hugombea kwa kupigiwa kura na kuingia kwenye baraza kwa kipindi cha miaka miwili.

Baraza hilo ndilo ambalo hupitisha maazimio yote ya muhimu ya UN kama kuwekwa kwa vikwazo na kutumika kwa nguvu za kijeshi.

Ili kupata nafasi hiyo nchi zinazogombea hufanya kampeni ya muda mrefu, huku Kenya ikiwa imefanikiwa kupata uungwaji mkono na Umoja wa Afrika.

Kunzia Januari 2021, nchi hiyo inakuwa kiungo muhimu na yenye nguvu katika Umoja wa Mataifa baada ya miaka 23 ambapo itahusika katika meza ya maamuzi muhimu duniani katika masuala ya amani na usalama.

Baadhi ya maamuzi hayo, Kenya inaweza kuhusika ni pamoja vikwazo, uidhinishaji wa utumiaji nguvu ili kuhakikisha Amani inadumu pamoja na kuchagua majaji katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ).

Kushirikiana pamoja na wanachama watano wa kudumu wa baraza hilo, zenye uwezo wa kupiga kura ya turufu ( Urusi, Uingereza, marekani, China na Ufaransa), Kenya itaungana na nchi zingine tisa wanachama wa baraza hilo wasio wa kudumu na huenda ikapata fursa ya kuwa mwenyekiti kwenye vikao vya baraza hilo, fursa muhimu ya kushinikiza ajenda.

Lakini kwa kuwa iliungwa mkono na AU, Kenya itakuwa na uhalali wa kulisemea bara la Afrika katika baraza hilo.

Kenya itaungana na Norway, Ireland, India na Mexico ambao walichaguliwa Jumatano.

Mchuano baina ya Kenya na Djibouti ilibidi uamuliwe Alhamisi jioni kwa saa za Marekani ili kumpata mshindi ambaye atachukua nafasi ya Afrika Kusini.

Nchi hizo zitahudumu kwa miaka miwili kuanzia 2021 mpaka 2023 ndani ya baraza hilo.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.