Star Tv

Burundi imemuapisha rais mpya wa taifa hilo , Evariste Ndayishimiye, katika hafla iliofanyika mbele ya raia wa taifa hilo na baadhi ya viongozi kutoka mataifa tofauti ikiwemo Tanzania.

Hafla hiyo imehudhuriwa na maelfu ya raia wa Burundi wamefurika katika uwanja huo wakisubiri kuapishwa kwa rais huyo kufuatia kifo cha aliyekuwa rais wa taifa hilo Pierre Nkurunziza.

Rais Ndayishimiye  ameapa kulinda katiba ya Burundi, kuheshimu umoja wa raia wa taifa hilo, kutoa haki kwa wote mbali na kutetea mipaka ya taifa hilo.

Kiapo hicho kinatokana na kifungu cha 107 cha katiba ya nchi hiyo Sherehe hiyo iliofanyika katika uwanja wa kandanda wa Ingoma katika mkoa wa Gitega imefanyika wakati ambapo taifa hilo limeathirika na mlipuko wa virusi vya corona.

Rais Evariste baada ya kumaliza kula kiapo alikagua gwaride la kijeshi na baadaye kutoa hotuba .

Aidha, muda mchache kabla ya kula kiapo rais Evariste aliombewa na baadhi ya maaskofu ambao walimtaka kufungua milango ya uhusiano mwema na mataifa mengine.

Latest News

AJALI YAUA WATU WATANO MKOANI DODOMA, WAWILI WAJERUHIWA.
03 Jul 2020 10:12 - Grace Melleor

Kamanda wa Polisi mkoani Dodoma Gilles Muroto amethibitisha kutokea kwa ajali ya gari aina ya Noah ambayo ilikuwa ikitok [ ... ]

ZTTO NA WENZAKE 07 WATAKIWA KUREJEA TENA POLISI.
01 Jul 2020 14:30 - Grace Melleor

Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo , Zitto Kabwe na viongozi wengine saba wa Chama hicho wameripoti Kituo Kikuu cha Pol [ ... ]

HALI YA MAAMBUKIZI YA CORONA YAWEZA KUWA MBAYA ZAIDI.
30 Jun 2020 13:13 - Grace Melleor

Mkuu wa shirika hilo, Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema virusi vinaweza kuathiri watu wengi zaidi kwa siku za usoni iki [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.