Star Tv

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe tayari amechukua fomu ya kuwania nafasi ya Urais katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwezi Oktoba 2020.

Licha ya Mwenyekiti huyo kuchukua fomu leo, Chama hicho pia leo Juni 17, 2020, kimetangaza majina ya Wanachama wake wengine walioomba kuteuliwa na Chama hicho kugombea nafasi ya Urais katika Uchaguzi Mkuu mwezi Oktoba.

Majina hayo yametajwa leo ambapo imesisitizwa kuwa mchakato wa awali ulikuwa unahusisha kuandika barua ya kutia nia na sio kuchukua na kurudisha fomu, hivyo watu walioandika barua kwa Katibu Mkuu John Mnyika ni 11.

Wanachama wengine waliokuwa wameshachukua fomu za kuwania kiti cha urais ni pamoja na Tundu Lissu na Peter Msigwa,Lazaro Nyalandu, Mwita Isaya, Dkt Majinge Mayrose, Manyama Leonard, Nicodemus Gasper, Nalo Opio, Neo Richmond na Shaaban Msafiri.

Aidha taarifa hiyo imefafanua kuwa kuna baadhi ya wanachama ambao wameelezwa kuwa ni bodaboda walijikusanya na kumwandikia barua mtu mmoja (ambaye hajatajwa) ili agombee lakini barua yao haikukidhi vigezo kutonana na kuwepo kwa sharti la mtu mwenyewe kuandika barua na sio kuandikiwa.

Latest News

AJALI YAUA WATU WATANO MKOANI DODOMA, WAWILI WAJERUHIWA.
03 Jul 2020 10:12 - Grace Melleor

Kamanda wa Polisi mkoani Dodoma Gilles Muroto amethibitisha kutokea kwa ajali ya gari aina ya Noah ambayo ilikuwa ikitok [ ... ]

ZTTO NA WENZAKE 07 WATAKIWA KUREJEA TENA POLISI.
01 Jul 2020 14:30 - Grace Melleor

Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo , Zitto Kabwe na viongozi wengine saba wa Chama hicho wameripoti Kituo Kikuu cha Pol [ ... ]

HALI YA MAAMBUKIZI YA CORONA YAWEZA KUWA MBAYA ZAIDI.
30 Jun 2020 13:13 - Grace Melleor

Mkuu wa shirika hilo, Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema virusi vinaweza kuathiri watu wengi zaidi kwa siku za usoni iki [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.