Star Tv

Jeshi la Korea Kaskazini limesema kwamba liko tayari kuingia katika eneo lisiloruhusiwa shughuli za kijeshi linalogawanya nchi hiyo na Korea Kusini ambapo Korea Kaskazini imetishia kutuma jeshi eneo salama la mpakani.

Tishio hilo linatokana na makundi yaliyoasi na kutorokea Korea Kusini yanayosambaza propaganda Korea Kaskazini.

Wikendi iliyoisha,Kim Yo-jong, dada wa kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong-un, alisema kwamba ataagiza jeshi kuelekea eneo hilo.

Na sasa hivi jeshi linasema liko tayari kubadilisha eneo hil kuwa ngome yao na kugusia kuwa liko macho.

Wasiwasi kati ya nchi hizo mbili umekuwa ukiongezeka kwa muda sasa kwasababu ya vipeperushi ambavyo vimekuwa vikisambaa katika mpaka wa maeneo hayo mawili ambavyo kawaida huwa vinatumwa kwa njia ya maputo.

Waziri wa ulinzi wa Korea Kusini Jumanne amejibu vitisho hivyo kwa kusema kuwa inashirikiana na Marekani kufuatilia kwa karibu hatua za kijeshi upande wa Korea Kaskazini.

Korea Kaskazini na Kusini zinagawanywa na eneo lisiloruhusiwa shughuli za kijeshi katika mpaka wake ambao umegawanya nchi hizo mbili tangu Vita ya Korea miaka ya 1950.

Jumanne, jeshi la Korea Kaskazini lilisema linafuatilia hatua inatakayochukuliwa na jeshi lake kwenda eneo hilo ambalo haliruhusiwi shughuli za kijeshi, huku Mkuu wa jeshi alisema liko katika hali ya tahadhari na tayari kutekeleza hatua yoyote itakayochukuliwa na serikali.

 

Latest News

AJALI YAUA WATU WATANO MKOANI DODOMA, WAWILI WAJERUHIWA.
03 Jul 2020 10:12 - Grace Melleor

Kamanda wa Polisi mkoani Dodoma Gilles Muroto amethibitisha kutokea kwa ajali ya gari aina ya Noah ambayo ilikuwa ikitok [ ... ]

ZTTO NA WENZAKE 07 WATAKIWA KUREJEA TENA POLISI.
01 Jul 2020 14:30 - Grace Melleor

Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo , Zitto Kabwe na viongozi wengine saba wa Chama hicho wameripoti Kituo Kikuu cha Pol [ ... ]

HALI YA MAAMBUKIZI YA CORONA YAWEZA KUWA MBAYA ZAIDI.
30 Jun 2020 13:13 - Grace Melleor

Mkuu wa shirika hilo, Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema virusi vinaweza kuathiri watu wengi zaidi kwa siku za usoni iki [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.