Star Tv

Chama cha Walimu Tanzania kimesema kinatambua jitihada kubwa ambazo zinafanywa na Serikali katika kuboresha maisha ya watanzania wakiwemo walimu, tunakupongeza pia kwa kuboresha Sekta ya Elimu - Katibu Mkuu wa CWT.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu CWT Deus Seif mbele ya JPM ambapo amesema kuwa wanamshukuru Rais kwa kuruhusu walimu kulipwa mishahara wakiwa nyumbani wakati huu wa ugonjwa wa Corona

“Tunashukuru Rais Magufuli kwa tamko lako la kuruhusu walimu kuendelea kulipwa mishahara tukiwa nyumbani wakati huu wa ugonjwa wa Corona” - Katibu Mkuu CWT, Deus Seif mbele ya JPM

Mbali na walimu kulipwa mshahara wakiwa nyumba CWT pia imempongeza Rais kwa kuhakikisha miundombinu ya thamani inapatikana katika mazingira ya kufundishia na kujifunzia, upandishaji wa madaraja pamoja na urekebishaji wa mishahara.

Aidha kwa upande wake rais Magufuli amesema kuwa bado ataendelea kuwalipa walimu mishara yao licha ya kwamba wako nyumbani;Corona hata ikikaa mwaka, hata ikikaa miaka 10 sitashindwa kuwalipa Walimu mishahara yao hata kama wako nyumbani, kwasababu Corona haikuletwa na Walimu lakini serikali inatambua mchango wa walimu"-Rais Magufuli.

Katika upande wengine Rais ametoa tamko la kuajiri walimu 13,526 kwa mwaka huu wa fedha unaoisha 2019/2020;

“Serikali inafahamu kwamba kuna upungufu wa walimu hususani wa hisabati , sayansi na lugha na hii ndio sababu katika kipindi cha miaka mitano iliyopita serikali imewaajiri walimu 22,341 na mwaka huu wa fedha unaoisha tutaajiri walimu wapya 13,526"-Rais Magufuli.”

Jumla ya wajumbe 1138 wameshiriki katika mkutano huu kutoka Mikoa 26 ya Tanzania Bara kwa ajili ya uchaguzi wa Viongozi wa Kitaifa wa Chama cha Walimu watakaoongoza kwa miaka mitano kuanzia mwaka 2020.

Latest News

AJALI YAUA WATU WATANO MKOANI DODOMA, WAWILI WAJERUHIWA.
03 Jul 2020 10:12 - Grace Melleor

Kamanda wa Polisi mkoani Dodoma Gilles Muroto amethibitisha kutokea kwa ajali ya gari aina ya Noah ambayo ilikuwa ikitok [ ... ]

ZTTO NA WENZAKE 07 WATAKIWA KUREJEA TENA POLISI.
01 Jul 2020 14:30 - Grace Melleor

Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo , Zitto Kabwe na viongozi wengine saba wa Chama hicho wameripoti Kituo Kikuu cha Pol [ ... ]

HALI YA MAAMBUKIZI YA CORONA YAWEZA KUWA MBAYA ZAIDI.
30 Jun 2020 13:13 - Grace Melleor

Mkuu wa shirika hilo, Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema virusi vinaweza kuathiri watu wengi zaidi kwa siku za usoni iki [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.