Star Tv

Mashetani wekundu wa Jiji la Manchester, Manchester United, inakaribia kuinasa saini ya beki wa Tottenham Hotspurs Toby Alderweireld kwa ada ya pauni milioni 60 na huenda dili hilo likafanikiwa ndani ya saa 48 zijazo baada ya mabosi wa timu zote mbili kuafikiana juu ya uhamisho huo.

Siku chache zilizopita, dili la uhamisho huo lilikwama kufuatia mabosi hao wa Red Devils kutokuwa tayari kutoa kitita cha pauni milioni 75 ambazo Spurs walihitaji ili waweze kumuachia mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 kuhamia viunga vya Old Traford, na sasa imeripotiwa kuwa mazungumzo baina ya mabosi wa timu zote mbili yameenda vizuri, kinachosubiriwa na mchezaji huyo kumwaga wino wa kukitumikia kikosi hicho kinachonolewa na Mreno Jose Mourinho kwa uhamisho wa pauni milioni 60.

Wakati dili la uhamisho huo likitegemewa kukamilika, United pia wapo katika hatua za mwisho za kupeleka ofa ya kutaka kumsajili kiungo mshambuliaji wa Chelsea, Willian mwenye umri wa miaka 29 ambaye kocha Jose Mourinho anaona kama silaha muhimu kuipata ili kuongeza nguvu kwenye safu ya ushambuliaji ya kikosi hicho kabla dirisha la usajili kufungwa majira haya ya kiangazi siku tano zijazo.

Mbrazili huyo ana mkataba unaomuweka Darajani hadi 20, lakini Mourinho anamchukulia mchezaji huyo kuwa chaguo lake namba moja kwenye dirisha hili la usajili. Hata hivyo wiki moja kabla, Mreno huyo alifanya mazungumzo na Mkurugenzi wa mashetani hao Ed Woodward, huku ikielezwa kuwa kocha huyo hafurahii namna klabu hiyo inavyoendesha zoezi la usajili huku kukiwa na sintofahamu juu ya kiungo wa kikosi hicho Mfaransa Paul Pogba kuendelea kubaki ndani ya viunga vya Old Traford baada ya wakala wake Mino Raiola kutaka mazungumzo na mabosi hao juu ya hatima yake, wakati huu ambapo Mabingwa wa La liga Barcelona wanamtolea macho. 

 

 

Latest News

Dkt. Jafo ofisi yake, imekamilisha taratibu zote za kupata Ithibati ya Kitabu ch...
24 Apr 2023 09:38 - Kisali Shombe

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo amewasilisha bungeni Hotuba ya Ma [ ... ]

TARI, Ukiruguru kuzindua Kifaa cha kupandia Mbegu cha Rafiki
23 Apr 2023 18:33 - Kisali Shombe

Sekta ya Kilimo ni mhimili wa uchumi wa Tanzania na imekuwa ikichangia Pato la mkulima mmoja mmoja, kaya na Taifa kwa uj [ ... ]

Wanawake kuwa sehemu ya Elimu dhidi ya Itikadi Kali na Ugaidi Afrika.
17 Apr 2023 10:28 - Kisali Shombe

Mnamo Oktoba 14, 2017, Mogadishu, Somalia ilikumbwa na shambulio baya la kigaidi lililoua watu 587 na kujeruhi zaidi ya  [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2023 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.