Star Tv

Kesi ya Uhujumu Uchumi namba 2 ya mwaka 2022 inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya ukiongozwa na Wakili Suzan Kimaro uliiambia Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi chini ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Salome Mshasha kuwa upelelezi wa kesi hiyo tayari ulikuwa umekamilika na kuomba tarehe nyingine kwa ajili ya kuwasilisha vibali maalumu kutoka ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini DPP.

Mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Moshi Erasto Phili upande wa Mashtaka umeieleza mahakama hiyo kuwa uko tayari kuwasilisha hati zote za kisheria kwa hakimu anayesikiliza kesi hiyo baada ya ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini DPP kuridhia Mahakama hiyo ianze kusikiliza shauri hilo.

Hata hivyo upande wa Utetezi ukiongozwa na Wakili Hellen Mahuna haukuwa na pingamizi lolote baada ya kujiridhisha kuwa Hakimu anayesikiliza Kesi alikuwa na udhuru hadi hapo atakaporejea.

Aidha umeomba shauri hilo kupangwa tarehe ya Karibu kwani mshtakiwa Lengai ole Sabaya kwa sasa anakabiliwa na maradhi ya Moyo. Baada ya kusikiliza pande zote mbili Hakimu Erasto Phili ameamuru shauri hilo kuletwa Mahakamani hapo Novemba 21 ya Mwaka huu na upande wa Mashtaka utawasilisha hati zote za Mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo Salome Mshasha. Lengai Ole Sabaya kwa Sasa bado anakabiliwa na shtaka la Uhukumu Uchumi lenye Mashtaka saba ikiwemo, utakatishaji wa Fedha, kuunda genge la kihalifu,Matumizi mabaya ya Madaraka.

Makosa ambayo yanadaiwa aliyatenda huko Bomang’ombe Wilayani Hai Mwaka 2021. Sabaya amerudishwa Rumande hadi Novemba 21 Mwaka huu.

Latest News

Waziri Mkuu Akagua Visima Vya Dharura Dar Es Salaam
10 Nov 2022 13:31 - Kisali Shombe

 WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekagua visima vya dharura vinavyosafishwa, kufufuliwa na kuunganishwa katika mfumo wa us [ ... ]

Waziri Wa Afya Aagiza Udhibiti Magonjwa Ya Mlipuko
09 Nov 2022 14:15 - Kisali Shombe

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ameagiza vituo vyote vya kutolea huduma za afya vya binafsi na serikali kuweka kituo maalum  [ ... ]

Vifo vitokanavyo na Utoaji wa Mimba usio salama, Kudhibitiwa
09 Nov 2022 13:21 - Kisali Shombe

Mpango wa idara ya afya wa kutoa elimu ya afya ya uzazi na matumizi ya uzazi wa mpango unatajwa kusaidia kupunguza mimba [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2023 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.