Maelfu ya waandamanaji wamejitokeza katika mitaa ya mji mkuu wa Tunisia kuandamana dhidi ya Rais wa nchi hiyo.
Maandamano kama hayo ya makundi ya kisiasa yanayopingana vikali yalifanyika mjini Tunis.
Makundi yote mawili yalimkashifu Rais Kais Saied kwa kuwa mbabe ambaye anabadilisha na kufifisha maendeleo ya kidemokrasia yaliyopatikana tangu ghasia za 2011.
Aidha pia waandamanaji hao walitaka uwajibikaji kutokana na mdodoro wa kiuchumi nchini humo ambao umeshuhudia uhaba mkubwa wa chakula na mafuta.
Wakosoaji wa Rais Saied wanamtuhumu kwa kufanya mapinduzi na kujaribu kurudisha Tunisia katika utawala wa kiimla mfumo wa serikali unaoendeshwa na mtu mmoja mwenye mamlaka kamili.
#ChanzoBBC