Star Tv

Polisi wa Urusi wameripotiwa kuwakamata mamia ya waandamanaji waliokuwa wakiandamana kupinga uamuzi wa Urusi wa kuongeza maelfu ya wanajeshi wa ziada kupigana nchini Ukraine.

Kikundi cha haki za binadamu cha Urusi OVD-Info kiliweka jumla ya idadi ya waliokamatwa kuwa zaidi ya 1,300.

Idadi kubwa zaidi ya waliokamatwa walikuwa raia wa St. Petersburg na Moscow.

Nchini Urusi, mikutano isiyoidhinishwa ni kinyume cha sheria chini ya sheria za kupinga maandamano.

Jana, ofisi ya mwendesha mashitaka ya Moscow ilionya kwamba wito kwenye mtandao wa kujiunga na maandamano yasiyoidhinishwa ya mitaani, au kushiriki katika maandamano hayo, inaweza kusababisha mwananchi kufungwa jela kwa miaka 15.

#ChanzoBBC

Latest News

MUHUDUMU MWINGINE AFARIKI KWA EBOLA UGANDA.
05 Oct 2022 12:44 - Grace Melleor

Wizara ya afya nchini Uganda imethibitisha kifo cha mhudumu mwingine wa afya, ambaye amefariki alfajiri ya leo Jumatano. [ ... ]

KIONGOZI MKUU WA IRAN AILAUMU MAREKANI NA ISRAEL.
04 Oct 2022 14:14 - Grace Melleor

Kiongozi mkuu wa Iran amezilaumu Marekani na Israel kwa kuchochea maandamano yaliyoenea nchini humo kufuatia kifo cha mw [ ... ]

WAHITIMU 1,384,340 KUANZA MTIHANI.
04 Oct 2022 13:56 - Grace Melleor

Jumla ya watahiniwa 1,384,340 wanatarajia kufanya mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi utakaofanyika Oktoba tano na sita  [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2022 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.