Star Tv

Jeshi la Polisi mkoa wa Arusha limefanikiwa kumkamata mtuhumiwa mmoja anayesafirisha madawa ya kulevya aina mirungi katika jiji la Arusha.

Akitoa taarifa hiyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishina msaidizi wa Polisi ACP. Justine Masejo amesema kuwa tarehe 21.09.2022 muda wa saa 03:20 asubuhi maeneo ya Njiro katika Halmashauri ya Jiji la Arusha Jeshi hilo limefanikiwa kumkamata mtu mmoja aitwaye Benson Emmanuel (28) Mkazi wa Ngaramtoni, wilaya ya Arumeru akiwa anakisafirisha madawa ya kulevya aina ya mirungi magunia 10 yenye uzito kilogramu 155.8.

Kamanda Masejo amebainisha kuwa Mtuhumiwa huyo alikamatwa akiwa anasafirisha madawa hayo ya kulevya kwa kutumia gari aina ya Toyota Rav 4 lenye namba za usajili T. 755 AWD huku akiwa amemwaga unga mweusi ambao unadhaniwa ni dawa za kienyeji kwa imani ya kutoonekana na vyombo vya ulinzi na usalama.

Aidha kamanda Masejo amewaambia waandishi wa Habari kuwa Uchunguzi wa awali wa Jeshi la Polisi umebaini kuwa mtuhumiwa huyo amekuwa akijihusisha na mtandao wa usafirishaji wa madawa ya kulevya.

Masejo ametoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Jeshi hilo kuhusiana na watu wachache wanaojihusisha na biashara haramu ya madawa ya kulevya ambayo yanaharibu vijana wengi na kupoteza nguvu kazi ya Taifa.

Latest News

MUHUDUMU MWINGINE AFARIKI KWA EBOLA UGANDA.
05 Oct 2022 12:44 - Grace Melleor

Wizara ya afya nchini Uganda imethibitisha kifo cha mhudumu mwingine wa afya, ambaye amefariki alfajiri ya leo Jumatano. [ ... ]

KIONGOZI MKUU WA IRAN AILAUMU MAREKANI NA ISRAEL.
04 Oct 2022 14:14 - Grace Melleor

Kiongozi mkuu wa Iran amezilaumu Marekani na Israel kwa kuchochea maandamano yaliyoenea nchini humo kufuatia kifo cha mw [ ... ]

WAHITIMU 1,384,340 KUANZA MTIHANI.
04 Oct 2022 13:56 - Grace Melleor

Jumla ya watahiniwa 1,384,340 wanatarajia kufanya mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi utakaofanyika Oktoba tano na sita  [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2022 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.