Star Tv

Uingereza, viongozi wa dunia na wafalme kote ulimwenguni wanatarajiwa leo kuuaga na kutoa heshima zao za mwisho kwa mwili wa Malkia Elizabeth wa pili.

Saa kumi na mbili na nusu asubuhi ya leo muda rasmi wa kuutazama mwili huo unafika kikomo baada ya siku nne zilizoshuhudia maelfu ya watu wakisimama kwenye foleni ndefu kuuona mwili wa malkia huyo katika ukumbi wa kihistoria wa Westminster jijini London. Mwendo wa saa tano jeneza lenye mwili wa Malkia Elizabeth litapelekwa hadi Westminster Abbey kwa ajili ya mazishi. Miongoni mwa watu 2,000 watakaohudhuria mazishi hayo watakuwemo viongozi 500 wa dunia akiwemo rais wa Marekani Joe Biden, Mfalme Naruhito wa Japan, makamu wa rais wa China, Wang Qishan na rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa. Vitukuu wa malkia, mwanamfalme George na binti mfalme Charlotte, watoto wawili wakubwa wa mrithi wa sasa wa kiti cha ufalme mwanamfalme William, pia watahudhuria.

CHANZO: DW SWAHILI

Latest News

MUHUDUMU MWINGINE AFARIKI KWA EBOLA UGANDA.
05 Oct 2022 12:44 - Grace Melleor

Wizara ya afya nchini Uganda imethibitisha kifo cha mhudumu mwingine wa afya, ambaye amefariki alfajiri ya leo Jumatano. [ ... ]

KIONGOZI MKUU WA IRAN AILAUMU MAREKANI NA ISRAEL.
04 Oct 2022 14:14 - Grace Melleor

Kiongozi mkuu wa Iran amezilaumu Marekani na Israel kwa kuchochea maandamano yaliyoenea nchini humo kufuatia kifo cha mw [ ... ]

WAHITIMU 1,384,340 KUANZA MTIHANI.
04 Oct 2022 13:56 - Grace Melleor

Jumla ya watahiniwa 1,384,340 wanatarajia kufanya mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi utakaofanyika Oktoba tano na sita  [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2022 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.