Star Tv

Serikali imezielekeza Halmashauri zote nchini kuanisha maeneo ya kimkakati ili ujenzi wa vituo vya afya vijengwe katika maeneo hayo na kurahisisha upatikanaji wa huduma za afya kwa wananchi.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia Afya Dkt. Festo Dugange wakati akijibu maswali bungeni leo kwa niaba ya Waziri wa Nchi wa Ofisi ya Raia TAMISEMI wakati akijibu swali la Mbunge wa Magu Kiswaga aliyetaka kujua lini Serikali itapeleka huduma ya vituo vya afya katika vijiji vya Lutale, Kwamanga na Igogo.

Dugange ameongeza kuwa Serikali ilishatoa utaratibu na kuzielekeza Halmashauri zote nchini kuanisha Kata za kimkakati kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya afya.

Ameongezea kuwa ujenzi wa vituo vya afya utazingatia vigezo na si kila eneo litajengwa vituo hivyo.

Aidha, ametoa wito kwa Mbunge na Mkurugenzi wa Halamshauri ya Wilaya Magu kushirikiana na Ofisi ya Rais – TAMISEMI kuangalia na kuanisha maeneo yenye vigezo hivyo ili hatua za haraka zichukuliwe ujenzi uanze na wananchi wapate huduma.

Mapema Naibu Waziri amewatoa hofu Waheshimiwa Wabunge kuwa, ujenzi wa vituo vya afya vitakavyojengwa ni pamoja na ununuzi wa vifaa tiba amesema, bajeti ya mwaka 2022/23 Serikali imetenga sh. bilioni 69.95 ambapo vifaa hivyo vitaenda kwenye vituo vya afya 530 vinavyojengwa nchi nzima.

“Ninapokea shukrani za Mbunge wa Rungwe Antony Mwantona kwa kazi kubwa iliyofanywa na Serikali kwa kujenga vituo vya afya vitatu ndani ya mwaka mmoja ndato, kimwa, imenjora” - Dugange

Aidha ameongeza kuwa, vituo vya afya vilivyokamilika vitapewa kipaumbele kwa kupatiwa vifaa tiba ili viweze kutoa huduma na wananchi waweze kupata huduma.

Dugange amesema, Serikali itaendelea kusimamia sekta ya afya na kuendelea kuweka mipango mizuri ili vituo vyote vinavyojengwa kuwekewa vifaatiba.

Latest News

MUHUDUMU MWINGINE AFARIKI KWA EBOLA UGANDA.
05 Oct 2022 12:44 - Grace Melleor

Wizara ya afya nchini Uganda imethibitisha kifo cha mhudumu mwingine wa afya, ambaye amefariki alfajiri ya leo Jumatano. [ ... ]

KIONGOZI MKUU WA IRAN AILAUMU MAREKANI NA ISRAEL.
04 Oct 2022 14:14 - Grace Melleor

Kiongozi mkuu wa Iran amezilaumu Marekani na Israel kwa kuchochea maandamano yaliyoenea nchini humo kufuatia kifo cha mw [ ... ]

WAHITIMU 1,384,340 KUANZA MTIHANI.
04 Oct 2022 13:56 - Grace Melleor

Jumla ya watahiniwa 1,384,340 wanatarajia kufanya mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi utakaofanyika Oktoba tano na sita  [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2022 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.