Star Tv

Wakati visa vya maambukizi ya Monkeypox vikiendelea kushuka kwenye mataifa ya Ulaya pamoja na Marekani, wataalam wa sayansi wanasema kwamba sasa ni wakati wa kuweka kipaumbele cha upatikanaji wa chanjo dhidi ya maradhi hayo barani Afrika.

Mwezi Julai, shirika la kimataifa la afya WHO liliorodhesha monkeypox kuwa dharura ya kimataifa, wakati likiomba jumuia ya kimataifa kusaidia mataifa ya kiafrika ili kuepuka ukosefu wa usawa wa chanjo, kama uliyoshuhudiwa wakati wa janga la Covid-19. Hata hivyo macho ya ulimwengu hayakuelekezewa kwenye bara hilo, huku kukikosa taifa hata moja tajiri lililotoa chanjo kwa ajili ya Afrika, wakati wataalam wakionya kwamba hamu ya kusaidia bara hilo huenda ikadidimia kabisa. Placide Mbala ambaye ni mtafiti wa magonjwa ya virusi kutoka taasisi ya kimatibabu ya Congo amesema kwamba hakuna lililobadilika kwa kuwa ulimwengu unashugulikia maambukizi ya monkeypox kwenye mataifa ya magharibi. Ameongeza kusema kwamba mataifa ya kiafrika ambako ugonjwa huo imekuwa kwa muda mrefu yamekuwa dhaifu ifikapo kwenye masuala ya utafiti, ufuatiliaji, upimaji pamoja na matibabu kwa wagonjwa. Monkeypox umeambukiza watu kwenye baadhi ya maeneo ya magharibi na kati mwa Afrika tangu miaka ya 70, lakini ulianza kuzungumziwa kwa kina baada ya kuzuka barani Ulaya na Marekani hivi karibuni, wataalam wa afya wakipendekeza kwa mara ya kwanza kutumika kwa chanjo dhidi yake. WHO imesema kwamba itaweka mikakati ya ugawaji wa chanjo ili kuhakikisha mataifa maskini yanazipata pia.

CHANZO: VOA SWAHILI

Latest News

MUHUDUMU MWINGINE AFARIKI KWA EBOLA UGANDA.
05 Oct 2022 12:44 - Grace Melleor

Wizara ya afya nchini Uganda imethibitisha kifo cha mhudumu mwingine wa afya, ambaye amefariki alfajiri ya leo Jumatano. [ ... ]

KIONGOZI MKUU WA IRAN AILAUMU MAREKANI NA ISRAEL.
04 Oct 2022 14:14 - Grace Melleor

Kiongozi mkuu wa Iran amezilaumu Marekani na Israel kwa kuchochea maandamano yaliyoenea nchini humo kufuatia kifo cha mw [ ... ]

WAHITIMU 1,384,340 KUANZA MTIHANI.
04 Oct 2022 13:56 - Grace Melleor

Jumla ya watahiniwa 1,384,340 wanatarajia kufanya mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi utakaofanyika Oktoba tano na sita  [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2022 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.