Star Tv

Shirika la ndege la Kenya Airways limethibitisha kuwa abiria aliyepata matatizo ya kupumua alipokuwa akipanda ndege kuelekea Mombasa nchini humo.

Katika taarifa KQ imesema abiria huyo alitangazwa kuwa amefariki katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) huku ndege hiyo iliyokuwa ikielekea Mombasa ikiwa bado ardhini.

“Kenya Airways PLC inasikitika kutangaza kwamba abiria alipata matatizo ya kupumua jioni hii alipokuwa akipanda KQ612 ambayo iliratibiwa kuondoka hadi Mombasa saa 1900. Abiria huyo alitangazwa kuwa amefariki na wafanyikazi wa matibabu katika JKIA wakati ndege ilikuwa ingali chini," - Taarifa ya KQ ilibainisha.

Shirika hilo mapema mwezi huu lilithibitisha kwamba abiria aliyekuwa kwenye mojawapo ya safari zake za ndege kuelekea New York kutoka Nairobi alikuwa ameaga dunia, ikiwa ni tukio la pili kama hilo kuripotiwa katika muda wa siku tisa.

Mwezi uliopita, iliripoti tukio lingine ambapo abiria alifariki kwenye mojawapo ya ndege zake kutoka New York kuelekea Nairobi.

Kulingana na shirika hilo la ndege, abiria huyo alipata matatizo ya kupumua saa saba baada ya ndege hiyo kupaa kutoka New York kabla ya kufariki. Msemaji wa familia alisema alikuwa na historia ya ugonjwa wa kisukari.

Latest News

MUHUDUMU MWINGINE AFARIKI KWA EBOLA UGANDA.
05 Oct 2022 12:44 - Grace Melleor

Wizara ya afya nchini Uganda imethibitisha kifo cha mhudumu mwingine wa afya, ambaye amefariki alfajiri ya leo Jumatano. [ ... ]

KIONGOZI MKUU WA IRAN AILAUMU MAREKANI NA ISRAEL.
04 Oct 2022 14:14 - Grace Melleor

Kiongozi mkuu wa Iran amezilaumu Marekani na Israel kwa kuchochea maandamano yaliyoenea nchini humo kufuatia kifo cha mw [ ... ]

WAHITIMU 1,384,340 KUANZA MTIHANI.
04 Oct 2022 13:56 - Grace Melleor

Jumla ya watahiniwa 1,384,340 wanatarajia kufanya mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi utakaofanyika Oktoba tano na sita  [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2022 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.