Star Tv

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula ametoa wito kwa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA) kuweka mpango wa matumizi ya ardhi katika eneo la Mradi wa wa Chanzo na Kituo cha Tiba ya Maji cha Butimba mkoani Mwanza.

Dkt Mabula ametoa wito huo wakati wa uwekaji jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa chanzo na kituo cha tiba ya Maji Butimba jijini Mwanza uliofanywa na Makamu wa Rais Dkt Phillip Isdori Mpango.

Ameishukuru MWAUWASA kwa kuweka uzio katika eneo linalozunguka mradi huo na kueleza kuwa, eneo hilo likiachwa wazi watu wataingia na ndipo migogoro ya ardhi inapoanza na kusisitiza kuwa mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza imefanya jambo zuri la kuweka uzio.

Aidha amesema pamoja na hatua ya kuwekwa uzio iliyofanywa na mamlaka hiyo lakini mpango wa matumizi bora ya ardhi kwenye eneo hilo ni muhimu ili kujua mahitaji ya huduma mbalimbali.

"Chanzo tunakiona kipo lakini wakiweka mpango wa matumizi mazuri kwenye eneo walilozungushia uzio tutajua tuna uhaba wa nyumba za watumishi zinazoweza kuwepo katika eneo hili na wakazi wake wakawa ni sehemu ya walinzi wa mradi. Uwepo wao utakuwa siyo tu utakuwa umeboresha maeneo lakini tutakuwa tumewapa makazi bora watumishi"- Dkt. Mabula.

Mradi wa ujenzi wa chanzo na kituo cha tiba ya maji Butimba umewekwa jiwe la msingi na Makamu wa Rais Dkt. Phillip Mpango ambapo katika hotuba yake ameagiza mradi huo kukamilika mapema Desemba 2022 ili iwe zawadi ya Krismas kwa wakazi wa jiji la Mwanza na kusisitiza wananchi wanaoishi eneo linalozunguka mradi ni lazima wapewe kipaumbele katika kupatiwa huduma ya maji.

Latest News

MUHUDUMU MWINGINE AFARIKI KWA EBOLA UGANDA.
05 Oct 2022 12:44 - Grace Melleor

Wizara ya afya nchini Uganda imethibitisha kifo cha mhudumu mwingine wa afya, ambaye amefariki alfajiri ya leo Jumatano. [ ... ]

KIONGOZI MKUU WA IRAN AILAUMU MAREKANI NA ISRAEL.
04 Oct 2022 14:14 - Grace Melleor

Kiongozi mkuu wa Iran amezilaumu Marekani na Israel kwa kuchochea maandamano yaliyoenea nchini humo kufuatia kifo cha mw [ ... ]

WAHITIMU 1,384,340 KUANZA MTIHANI.
04 Oct 2022 13:56 - Grace Melleor

Jumla ya watahiniwa 1,384,340 wanatarajia kufanya mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi utakaofanyika Oktoba tano na sita  [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2022 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.