Star Tv

Mwanasiasa wa Kenya William Ruto ataapishwa leo kuwa rais wa tano wa taifa hilo wiki moja baada ya Mahakama ya Juu nchini humo kutupilia mbali shauri la kupinga matokeo ya uchaguzi wa Agosti 9 yaliyompa ushindi.

Ruto ataanza muhula wake wa miaka mitano chini ya changamoto za kupanda kwa bei ya vyakula na nishati pamoja na kiwingu cha ukosefu mkubwa wa ajira na deni la taifa linaongezeka kwa kasi.Mwanasiasa huyo ambaye kwa miaka kumi iliyopita alikuwa makamu wa rais chini ya rais anayondoka madarakani Uhuru Kenyatta, alipata ushindi mwembamba katika uchaguzi wa mwezi Agosti akimbwaga kiongozi wa muda mrefu wa upinzani Raila Odinga.Wakati wa uchaguzi huo, Odinga alikuwa akiungwa mkono na rais Kenyatta ambaye katika miaka ya karibuni alitumbukia kwenye msuguano na Ruto kutokana na sababu za kisiasa.

CHANZO: DW SWAHILI

Latest News

MUHUDUMU MWINGINE AFARIKI KWA EBOLA UGANDA.
05 Oct 2022 12:44 - Grace Melleor

Wizara ya afya nchini Uganda imethibitisha kifo cha mhudumu mwingine wa afya, ambaye amefariki alfajiri ya leo Jumatano. [ ... ]

KIONGOZI MKUU WA IRAN AILAUMU MAREKANI NA ISRAEL.
04 Oct 2022 14:14 - Grace Melleor

Kiongozi mkuu wa Iran amezilaumu Marekani na Israel kwa kuchochea maandamano yaliyoenea nchini humo kufuatia kifo cha mw [ ... ]

WAHITIMU 1,384,340 KUANZA MTIHANI.
04 Oct 2022 13:56 - Grace Melleor

Jumla ya watahiniwa 1,384,340 wanatarajia kufanya mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi utakaofanyika Oktoba tano na sita  [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2022 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.