Star Tv

Mahakama ya Juu Kenya kutoa uamuzi kuhusu uchaguzi wa rais Kenya Mahakama ya juu nchini Kenya itatoa uamuzi wake leo wa kama itaidhinisha au kubatilisha matokeo ya uchaguzi wa rais wa mwezi uliopita.

Mahakama hiyo yenye majaji saba itatoa uamuzi baada ya wiki iliyopita kusikiliza kwa siku tatu hoja za mawakili wanaowasimamia wagombea wawili wakuu na makundi pinzani ya makamishena wa tume ya uchaguzi. William Ruto, ambaye alitangazwa mshindi wa uchaguzi huo wa Agosti 9, amesema jana kuwa ataheshimu uamuzi wa Mahakama ya Juu kwa sababu Kenya ni nchi inayofuata utawala wa kisheria. Ruto ambaye ni naibu wa rais, alitangazwa mshindi na tume ya uchaguzi kwa kupata asilimia 50.49 dhidi ya asilimia 48.85 ya kiongozi mkongwe Raila Odinga aliyeungwa mkono na Rais Uhuru Kenyatta. Odinga alipinga matokeo hayo na kuwasilisha kesi katika Mahakama ya Upeo akidai kulikuwa na udanganyifu katika mchakato wa kuhesabu kura. Mgombea mwenza wa Odinga, Martha Karua alisema muungano wao wa Azimio One Kenya pia utaheshimu uamuzi wa leo.

CHANZO: DW SWAHILI

Latest News

MUHUDUMU MWINGINE AFARIKI KWA EBOLA UGANDA.
05 Oct 2022 12:44 - Grace Melleor

Wizara ya afya nchini Uganda imethibitisha kifo cha mhudumu mwingine wa afya, ambaye amefariki alfajiri ya leo Jumatano. [ ... ]

KIONGOZI MKUU WA IRAN AILAUMU MAREKANI NA ISRAEL.
04 Oct 2022 14:14 - Grace Melleor

Kiongozi mkuu wa Iran amezilaumu Marekani na Israel kwa kuchochea maandamano yaliyoenea nchini humo kufuatia kifo cha mw [ ... ]

WAHITIMU 1,384,340 KUANZA MTIHANI.
04 Oct 2022 13:56 - Grace Melleor

Jumla ya watahiniwa 1,384,340 wanatarajia kufanya mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi utakaofanyika Oktoba tano na sita  [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2022 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.