Star Tv

Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud ameahidi kutokomeza kundi la Al Shabab katika taarifa yake ya kwanza kwa taifa tangu wanamgambo hao wa Kiislamu kufanya uvamizi mbaya wa saa 30 kwenye hoteli moja mjini Mogadishu.

Shambulio hilo ambalo lilianza Ijumaa jioni, lilikuwa ndilo kubwa zaidi kukumba mji mkuu wa Somalia tangu Mohamud aingie madarakani mwezi Juni na kusisitiza changamoto ya kujaribu kumaliza uasi wa miaka 15 wa kundi lenye uhusiano na Al-Qeada.

Watu 21 walifariki na wengine 117 kujeruhiwa katika shambulio hilo la bunduki na mabomu lililolenga hoteli maarufu ya Hayat, na raia wa Norway ni miongoni mwa waliokufa, kwa mujibu wa serikali ya Norway.

“Ninajua kwamba wananchi wa Somalia wamechoshwa na rambirambi na maombolezo yasiyoisha, najua kwamba mnawapoteza watu wenye thamani katika kila shambulio linolafanywa na magaidi,” Mohamud amesema.

Rais Mohamud amebainisha kwamba,
“Tuna dhamira ya kuwadhoofisha magaidi wanaoteketeza wananchi wetu hadi maeneo yote wanayoyadhibiti yamekombolewa, hili ni jambo la kipaumbele kwa serikali yetu na maandalizi na utelekelezaji wa mpango huo unaendelea,”.

#ChanzoVOASwahili

Latest News

MUHUDUMU MWINGINE AFARIKI KWA EBOLA UGANDA.
05 Oct 2022 12:44 - Grace Melleor

Wizara ya afya nchini Uganda imethibitisha kifo cha mhudumu mwingine wa afya, ambaye amefariki alfajiri ya leo Jumatano. [ ... ]

KIONGOZI MKUU WA IRAN AILAUMU MAREKANI NA ISRAEL.
04 Oct 2022 14:14 - Grace Melleor

Kiongozi mkuu wa Iran amezilaumu Marekani na Israel kwa kuchochea maandamano yaliyoenea nchini humo kufuatia kifo cha mw [ ... ]

WAHITIMU 1,384,340 KUANZA MTIHANI.
04 Oct 2022 13:56 - Grace Melleor

Jumla ya watahiniwa 1,384,340 wanatarajia kufanya mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi utakaofanyika Oktoba tano na sita  [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2022 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.