Star Tv

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema taifa lake linahitaji silaha nyingi zaidi zitakazowasaidia kupambana na Urusi.

Katika hotuba yake ya kila Jumamosi, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesisitiza haja ya nchi yake kupatiwa silaha.

“Tunafanya kazi kila siku kuimarisha ulinzi wetu. Hii kimsingi ni kupata silaha, Bila shaka, kwa kiwango kikubwa inategemea na washirika wetu. Kwa utayari wao wakuipatia Ukraine kila kilicho muhimu kulinda uhuru wetu.”

Gazeti la New York Times limeripoti kwamba Ukraine “imepatiwa silaha na Denmark makombora ya Harpoon ya kujilinda na mashambulizi ya manowari za kivita,”.

Majeshi ya Urusi tayari yametangaza kuwa yameuchukua mji wa mashariki mwa Ukraine wa Lyman, kituo kikuu cha treni katika mkoa wa Donetsk. Kutekwa kwa mji huo kunaashiria mabadiliko ya kasi ya vita huko Ukraine.

 

Gavana wa mkoa Luhansk, ambao pamoja na Donetsk unaunda Donbas, alisema Ijumaa kuwa vikosi vya Urusi vimeingia Sievierodonetsk.

Latest News

RAIS WA UKRAINE AAMURU RAIA WOTE KUHAMA MKOA WA DONETSK.
31 Jul 2022 17:17 - Grace Melleor

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ameamuru raia wote ambao bado wanaishi katika maeneo ya mashariki mwa mkoa wa Donetsk [ ... ]

KIFO CHA RAIA WA NIGERIA NCHINI ITALIA CHAZUA HASIRA.
31 Jul 2022 16:58 - Grace Melleor

Kifo cha mhamiaji aliyeshambuliwa mchana kweupe nchini Italia kimezua hasira.

VUTA N’KUVUTE YA MANARA NA KATIBU WA TFF YAIBUKA.
25 Jul 2022 16:37 - Grace Melleor

Katibu Mkuu wa Shrikishi la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Kidao Wilfred amesema amesekitishwa na madai ya yaliyekuwa Af [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2022 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.