Star Tv

Rais wa Senegal Macky Sall amesema atasafiri hadi Urusi na Ukraine hivi karibuni katika wadhifa wake kama mwenyekiti wa sasa wa Umoja wa Afrika kwa lengo la kuzuru nchi hizo mbili.

Sall amesema kwamba hapo jana jumapili Mei 22,2022 amepokea mamlaka ya wakuu wengine wa nchi wa AU kufanya safari hizo.

Katika mkutano wa pamoja na Kansela wa Ujerumani anayezuru Afrika Olaf Sholz, amesema Afrika ina nia ya kuona amani kupitia mazungumzo kati ya Ukraine na Urusi.

Rais huyo wa Senegal amesema Urusi imetoa mwaliko wa kufanya ziara huku rais wa Ukraine akieleza haja ya kuwasiliana na wakuu wa nchi za Afrika.

Mgogoro wa Urusi na Ukraine umekatiza usambazaji wa nafaka na mafuta ya kupikia, na hivyo kuzidisha uhaba wa chakula hasa katika nchi maskini za Afrika kutokana na kupanda kwa bei na pia bei ya mafuta duniani imepanda kutokana na hilo.

Latest News

MUHUDUMU MWINGINE AFARIKI KWA EBOLA UGANDA.
05 Oct 2022 12:44 - Grace Melleor

Wizara ya afya nchini Uganda imethibitisha kifo cha mhudumu mwingine wa afya, ambaye amefariki alfajiri ya leo Jumatano. [ ... ]

KIONGOZI MKUU WA IRAN AILAUMU MAREKANI NA ISRAEL.
04 Oct 2022 14:14 - Grace Melleor

Kiongozi mkuu wa Iran amezilaumu Marekani na Israel kwa kuchochea maandamano yaliyoenea nchini humo kufuatia kifo cha mw [ ... ]

WAHITIMU 1,384,340 KUANZA MTIHANI.
04 Oct 2022 13:56 - Grace Melleor

Jumla ya watahiniwa 1,384,340 wanatarajia kufanya mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi utakaofanyika Oktoba tano na sita  [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2022 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.