Star Tv

Rais wa Marekani Joe Biden alitia saini Sheria ya Kukodisha kwa Mkopo, iliyoundwa ili kurahisisha utaratibu wa kusambaza silaha kwa Ukraine.

Hati hivyo, kipengele hicho kilichopewa jina la "Sheria ya Kukodisha, Kulinda Demokrasia nchini Ukraine ya 2022," iliwasilishwa kwa Bunge la Congress hata kabla ya kuanza kwa uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, Januari mwaka huu.

Mnamo Mei 3, muswada huo uliidhinishwa kwa kura nyingi za Baraza la Wawakilishi la Bunge la Marekani (417 waliunga mkono, 10 walipinga), na kabla ya hapo muswada huo uliidhinishwa na Seneti.

Kwa mujibu wa muswada huo, Rais wa Marekani "anaweza kuidhinisha serikali kukopesha au kukodisha mali ya ulinzi kwa Ukraine na nchi nyingine za Ulaya Mashariki zilizoathiriwa na uvamizi wa Urusi nchini Ukraine ili kusaidia kuimarisha ulinzi wa nchi hizi na kulinda raia dhidi ya mashambulizi yanayoweza kutokea au kuendelea".

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ameishukuru Marekani na Biden kwa kufufua mpango wa msaada. "Asante @POTUS na watu wa Marekani kwa kuunga mkono Ukraine katika kupigania uhuru na mustakabali wetu," akaunti rasmi ya rais wa Ukraine ilituma ujumbe huo kupitia Twitter.

Wakati wa Vita vya Kidunia vya pili, mmoja wa wapokeaji wakuu wa misaada kama hiyo alikuwa Umoja wa Kisovieti.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alishukuru Marekani na Biden kwa kufufua mpango wa msaada. "Asante @POTUS na watu wa Marekani kwa kuunga mkono Ukraine katika kupigania uhuru na mustakabali wetu," akaunti rasmi ya rais wa Ukrain ilituma ujumbe huo kupitia Tiwtter kwa Kiingereza.

#ChanzoBBC

 

 

Latest News

AMPELEKA MKWE MAHAKAMANI KWA KUMZUIA KUOLEWA.
17 May 2022 06:34 - Grace Melleor

Binti aliyefahamika kwa jila la Halima Yunusa Ibrahim amempeleka babamkwe wake latika Mahakama ya Kiislamu Islamic (Shar [ ... ]

WANAJESHI WA UKRAINE WALIOZINGIRWA WALIOKOLEWA.
17 May 2022 05:50 - Grace Melleor

Ukraine imethibitisha kwamba mamia ya wapiganaji wake waliokuwa wamekwama kwa zaidi ya miezi miwili katika mji wa Maurip [ ... ]

JESHI LA NATO KUANZA KUFANYA MAZOEZI KUKABILI VITA.
16 May 2022 09:23 - Grace Melleor

Mazoezi makubwa zaidi katika historia ya Baltics ya Muungano wa kijeshi wa NATO yanatarajiwa kuanza baadaye hii leo.

Other Articles

Social Media

Copyright © 2022 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.