Star Tv

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Innocent Bashungwa amemuelekeza Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Amos Makalla kusimamia usitishwaji wa zuio la bodaboda na bajaji kuingia katikati ya Jiji la Dar es Salaam.

Bashungwa amechukua hatua hiyo kufuatia uamuzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam la kupiga marufuku bodaboda na bajaji kuingia katikati ya Jiji la Dar es Salaam isipokuwa maeneo yaliyoainishwa.

"Bila shaka nia ni njema, ila dosari ipo kwenye handling (kushughulikia) ya jambo lenyewe. Serikali yetu ya Awamu ya Sita inatambua na kuthamini ajira za vijana wetu za bodaboda na bajaji kuwa ni ajira rasmi na wanajipatia riziki na familia zao. Namuelekeza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Amos Makalla kusimamia usitishwaji wa zuio hilo ili kutoa nafasi ya kufanya tafakuri zaidi."- Amesema Bashungwa.

Tangazo la kusitisha kwa vyombo hivyo vya usafiri kuingia katikati ya Jiji lilitolewa jana Aprili 20, 2022

Latest News

RAIS WA UKRAINE AAMURU RAIA WOTE KUHAMA MKOA WA DONETSK.
31 Jul 2022 17:17 - Grace Melleor

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ameamuru raia wote ambao bado wanaishi katika maeneo ya mashariki mwa mkoa wa Donetsk [ ... ]

KIFO CHA RAIA WA NIGERIA NCHINI ITALIA CHAZUA HASIRA.
31 Jul 2022 16:58 - Grace Melleor

Kifo cha mhamiaji aliyeshambuliwa mchana kweupe nchini Italia kimezua hasira.

VUTA N’KUVUTE YA MANARA NA KATIBU WA TFF YAIBUKA.
25 Jul 2022 16:37 - Grace Melleor

Katibu Mkuu wa Shrikishi la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Kidao Wilfred amesema amesekitishwa na madai ya yaliyekuwa Af [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2022 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.