Star Tv

Watu sita wamefariki dunia na wengine wanne wamejeruhiwa katika ajali iliyohusisha gari aina ya Toyota Noah iliyogongana na lori aina ya scania katika eneo la ALKATANI kata ya Sepeko tarafa ya Kisongo wilaya ya Monduli mkoa wa Arusha katika barabara ya Arusha Babati.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha ACP. Justine Masejo amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambapo amesema ajali hiyo imetokea jana Aprili 19, 2022 muda wa saa nne usiku na kuyataja magari hayo kuwa ni Toyota Noah yenye namba za usajili T.189 DFY iliyokuwa ikitokea Arusha mjini kwenda Karatu na lori lenye namba za usajili T.250 CAA ambapo lori hilo lilikuwa linatokea makuyuni kwenda Arusha mjini.

ACP. Masejo amesema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva ambapo alishindwa kulimudu gari hilo na kuhamia upande mwingine wa Barabara na kusabisha kugonga gari hilo aina ya toyota Noah. Kamanda Masejo amesema kuwa Jeshi hilo linamshikilia dereva wa roli aliyesababisha ajali hiyo.

Aidha amesema kuwa bado wanaendelea kufanya uchunguzi kufahamu majina halisi ya abiria waliofariki katika ajali hiyo na amewaomba wananchi kufika katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Arusha Mount Meru kutambua miili ya marehemu.

ACP. Masejo ametoa wito kwa watumiaji wa vyombo vya moto kuwa waangalifu wakati wamatumizi ya vyombo hivyo ili kupunguza ajali ambazo zinagharimu maisha ya watu.

Latest News

RAIS WA UKRAINE AAMURU RAIA WOTE KUHAMA MKOA WA DONETSK.
31 Jul 2022 17:17 - Grace Melleor

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ameamuru raia wote ambao bado wanaishi katika maeneo ya mashariki mwa mkoa wa Donetsk [ ... ]

KIFO CHA RAIA WA NIGERIA NCHINI ITALIA CHAZUA HASIRA.
31 Jul 2022 16:58 - Grace Melleor

Kifo cha mhamiaji aliyeshambuliwa mchana kweupe nchini Italia kimezua hasira.

VUTA N’KUVUTE YA MANARA NA KATIBU WA TFF YAIBUKA.
25 Jul 2022 16:37 - Grace Melleor

Katibu Mkuu wa Shrikishi la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Kidao Wilfred amesema amesekitishwa na madai ya yaliyekuwa Af [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2022 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.