Star Tv

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amezitaka taasisi za fedha kubuni mikakati na mbinu zitakazowezesha watanzania wengi zaidi kupata huduma rasmi za kibenki kwa gharama nafuu ili waweze kujiongezea kipato na kujikwamua na umasikini.

Majaliwa ametoa wito huo leo Jumatatu Aprili 11, 2022, katika hafla ya huduma ya Teleza Kidijitali inayotolewa na Benki ya NMB, iliyofanyika jijini Dodoma, Ambapo amezishauri taasisi nyingine za kifedha ziige utoaji wa huduma kwa njia hiyo.

Waziri Mkuu amesema kuwa taasisi hizo hazina budi kuiunga mkono Serikali kwa kubuni mikakati mbalimbali ya kuhamasisha matumizi ya teknolojia katika kukuza uchumi sambamba na kubuni masuluhisho rahisi kwa watumiaji wa kawaida.

Aidha, amesema benki nchini hazina budi kubuni zaidi namna ya kutafuta masuluhusho yaliyo katika sekta za kifedha. “Hongereni NMB kwa ubunifu huu ambao utavutia makundi yote ya kijamii, huduma hii itawezesha wateja wenu kupata huduma ya mikopo kiganjani.”

Latest News

RAIS WA UKRAINE AAMURU RAIA WOTE KUHAMA MKOA WA DONETSK.
31 Jul 2022 17:17 - Grace Melleor

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ameamuru raia wote ambao bado wanaishi katika maeneo ya mashariki mwa mkoa wa Donetsk [ ... ]

KIFO CHA RAIA WA NIGERIA NCHINI ITALIA CHAZUA HASIRA.
31 Jul 2022 16:58 - Grace Melleor

Kifo cha mhamiaji aliyeshambuliwa mchana kweupe nchini Italia kimezua hasira.

VUTA N’KUVUTE YA MANARA NA KATIBU WA TFF YAIBUKA.
25 Jul 2022 16:37 - Grace Melleor

Katibu Mkuu wa Shrikishi la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Kidao Wilfred amesema amesekitishwa na madai ya yaliyekuwa Af [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2022 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.