Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis, ametoa wito wa kusitishwa kwa vita nchini Ukraine na kufungua njia ya amani kupitia "majadiliano ya kweli".
Akihutubia misa ya Jumapili jana Aprili 10, kwenye Uwanja wa kanisa la Mtakatifu Peter mjini Vatican, Papa Francis amesema kuna haja ya kuwepo usitishwaji mapigano utakaoleta amani badala ya kusambaza zaidi silaha.
Siku ya Jumatano, Papa Francis alilaani kulengwa kwa raia nchini Ukraine, akisema kugundulika kwa maiti za watu huko Bucha ni mauaji ya kinyama.
Ameelezea pia nia yake ya kutoa mchango katika kusitisha mapigano nchini Ukraine, akisema yupo tayari kufanya ziara mjini Kyiv.
#ChanzoDW