Star Tv

Benki ya Dunia imesema inatarajia uchumi wa Ukraine utapungua kwa 45% mwaka huu kutokana na vita.

Benki hiyo imetabiri pia kuwa kutakuwa na uharibifu mkubwa wa kiuchumi kuliko uliosababishwa na janga la Covid-19 kote Ulaya mashariki na Asia ya kati, na vikwazo ambavyo havijawahi kushuhudiwa na kusababisha mdororo mkubwa wa uchumi nchini Urusi pia.

Sehemu kubwa ya wafanyakazi wa Ukraine wamelazimika kukimbia na biashara nyingi zimefungwa, huku barabara, viwanda na miundombinu mingine ikiharibiwa.

Benki ya Dunia imebainisha pia juu ya maendeleo ya miaka mingi ya nchi hiyo ikisema yamebatilishwa. "Ukraine ilikuwa chanzo kikuu cha mazao kama vile alizeti na ngano lakini kutokana na mauzo ya nje kusitishwa bei ya vyakula duniani imepanda".

Vikwazo dhidi ya Urusi vinamaanisha kuwa benki ya Dunia inatabiri uchumi wake kupungua zaidi ya 11% mwaka huu.

#ChanzoBBC

Latest News

AMPELEKA MKWE MAHAKAMANI KWA KUMZUIA KUOLEWA.
17 May 2022 06:34 - Grace Melleor

Binti aliyefahamika kwa jila la Halima Yunusa Ibrahim amempeleka babamkwe wake latika Mahakama ya Kiislamu Islamic (Shar [ ... ]

WANAJESHI WA UKRAINE WALIOZINGIRWA WALIOKOLEWA.
17 May 2022 05:50 - Grace Melleor

Ukraine imethibitisha kwamba mamia ya wapiganaji wake waliokuwa wamekwama kwa zaidi ya miezi miwili katika mji wa Maurip [ ... ]

JESHI LA NATO KUANZA KUFANYA MAZOEZI KUKABILI VITA.
16 May 2022 09:23 - Grace Melleor

Mazoezi makubwa zaidi katika historia ya Baltics ya Muungano wa kijeshi wa NATO yanatarajiwa kuanza baadaye hii leo.

Other Articles

Social Media

Copyright © 2022 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.