Star Tv

Mahakama ya kijeshi nchini Burkina Faso imemuhukumu rais wa zamani Blaise Compaore kifungo cha maisha gerezani kwa kuhusika katika mauaji ya mtangulizi wake Thomas Sankara mwaka 1987.

Compaore, ambaye yuko uhamishoni, amehukumiwa kifungo hicho bila kuwepo.

Mkuu wake wa usalama, Hyacinthe Kafando, pia amehukumiwa kifungo cha Maisha jela.

Bwana Sankara, mwanamapinduzi aliyekuwa na itikadi za Kimarxist, aliuawa kwa kupigwa risasi na kundi la watu wenye silaha katika mji mkuu, Ouagadougou mwaka 1987.

Baada ya mauji hayo Compaore alitawala kwa miaka 27 kabla ya kupinduliwa mwaka 2014.

#ChanzoBBC

Latest News

AMPELEKA MKWE MAHAKAMANI KWA KUMZUIA KUOLEWA.
17 May 2022 06:34 - Grace Melleor

Binti aliyefahamika kwa jila la Halima Yunusa Ibrahim amempeleka babamkwe wake latika Mahakama ya Kiislamu Islamic (Shar [ ... ]

WANAJESHI WA UKRAINE WALIOZINGIRWA WALIOKOLEWA.
17 May 2022 05:50 - Grace Melleor

Ukraine imethibitisha kwamba mamia ya wapiganaji wake waliokuwa wamekwama kwa zaidi ya miezi miwili katika mji wa Maurip [ ... ]

JESHI LA NATO KUANZA KUFANYA MAZOEZI KUKABILI VITA.
16 May 2022 09:23 - Grace Melleor

Mazoezi makubwa zaidi katika historia ya Baltics ya Muungano wa kijeshi wa NATO yanatarajiwa kuanza baadaye hii leo.

Other Articles

Social Media

Copyright © 2022 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.