Star Tv

Wapinzani wa Sudan Kusini wametia saini makubaliano ya kuunda kamandi ya jeshi la pamoja, nguzo muhimu ya makubaliano ya amani yaliyotiwa saini mwaka 2018.

Mkataba huo ulitiwa saini siku ya Jumapili katika mji mkuu, Juba, kufuatia upatanishi wa nchi jirani ya Sudan.

Mvutano kati ya Rais Salva Kiir na Makamu wa Kwanza wa Rais Riek Machar hivi karibuni ulisababisha mapigano kati ya vikosi vyao.

Makubaliano hayo yanaweka masharti ya kuwajumuisha makamanda wa upinzani katika vikosi vya jeshi.

Mrengo wa Rais Kiir utakuwa na uwakilishi wa 60% katika nyadhifa muhimu katika jeshi, polisi na vikosi vya usalama. SPLM-IO ya Bw Machar na makundi mengine ya upinzani yatachukua asilimia 40 iliyobaki.

Upinzani utawasilisha orodha ya makamanda wao ndani ya kipindi cha wiki moja.Itafuatiwa na kuhitimu kwa vikosi vya umoja na kutumwa kwao - ambayo haipaswi kuzidi muda wa miezi miwili, kulingana na mpango huo."Watu wa Sudan Kusini wanatamani amani na amani inahusu usalama na leo tumepiga hatua kubwa katika hilo.

Tumekubaliana kwamba tutasonga mbele,” amesema Meja Jenerali Martin Abucha, aliyewakilisha mrengo wa Bw Machar.

“Ninataka kutoa wito kwa wenzangu kutoka pande nyingine kwamba ni muhimu kunyamazisha milio ya bunduki ili Sudan Kusini ifanikiwe. Kusiwe na mapigano, kusiwe na mashambulizi”.

Aidha Mamlaka ya Kiserikali ya Maendeleo (Igad), imesifu mpango huo kama "mafanikio makubwa".

#ChanzoBBC

 

 

Latest News

AMPELEKA MKWE MAHAKAMANI KWA KUMZUIA KUOLEWA.
17 May 2022 06:34 - Grace Melleor

Binti aliyefahamika kwa jila la Halima Yunusa Ibrahim amempeleka babamkwe wake latika Mahakama ya Kiislamu Islamic (Shar [ ... ]

WANAJESHI WA UKRAINE WALIOZINGIRWA WALIOKOLEWA.
17 May 2022 05:50 - Grace Melleor

Ukraine imethibitisha kwamba mamia ya wapiganaji wake waliokuwa wamekwama kwa zaidi ya miezi miwili katika mji wa Maurip [ ... ]

JESHI LA NATO KUANZA KUFANYA MAZOEZI KUKABILI VITA.
16 May 2022 09:23 - Grace Melleor

Mazoezi makubwa zaidi katika historia ya Baltics ya Muungano wa kijeshi wa NATO yanatarajiwa kuanza baadaye hii leo.

Other Articles

Social Media

Copyright © 2022 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.