Star Tv

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametangaza uamuzi wa Serikali wa kuondoa tozo 42 kati ya 47 ambazo walikuwa wanatozwa wakulima wa kahawa wa Mkoa wa Kagera hadi kufikia tozo 5 tu ambazo itakuwa ni jumla ya Shilingi 267 kwa kila kilo ya kahawa, kutoka Shilingi 830 za awali.

Waziri Mkuu ametoa maamuzi hayo kufuatia tume maalum aliyoiunda ili kupitia utaratibu na mfumo wa uendeshaji wa vyama vya Ushirika wa zao la kahawa Mkoani Kagera.

Waziri Mkuu ametoa maagizo hayo leo Machi 29, 2022 Wakati alipoendesha Mkutano Maalum wa Wadau wa zao la kahawa mkoani Kagera uliofanyika wilayani Karagwe Mkoa wa Kagera.

Majaliwa amewaagiza viongozi wa vyama vya Ushirika, wasimamie vyama vyao kwa uaminifu na weledi ili vilete tija kwa wakulima na amewataka viongozi wa vyama vikuu vya ushirika kuacha tabia ya kukopa pesa benki kwa ajili ya kununua kahawa kwa wakulima.

Amesema kuanzia sasa mauzo ya kahawa katika Mkoa wa Kagera yatafanyika kwa njia ya mnada. “Mnada huo utafanyika kwenye ngazi ya vyama vya msingi.”

Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amesema baadhi ya vyama vya ushirika vimekuwa vikiwaumiza wakulima wa kahawa kwa kuwaongezea tozo zisizokuwa na tija.

Amesema jambo hilo linafanyiwa kazi kwani wakulima wa kahawa mkoani Kagera wamekuwa wakilia na tozo kubwa zaidi ya 47 na bado wamekuwa wakicheleweshewa malipo.

Waziri huyo amemuagiza Mkurugenzi wa Bodi ya Kahawa kugawa miche ya kutosha ya kahawa kwa wakulima ili ilete tija na kuwaongezea kipato.

Latest News

AMPELEKA MKWE MAHAKAMANI KWA KUMZUIA KUOLEWA.
17 May 2022 06:34 - Grace Melleor

Binti aliyefahamika kwa jila la Halima Yunusa Ibrahim amempeleka babamkwe wake latika Mahakama ya Kiislamu Islamic (Shar [ ... ]

WANAJESHI WA UKRAINE WALIOZINGIRWA WALIOKOLEWA.
17 May 2022 05:50 - Grace Melleor

Ukraine imethibitisha kwamba mamia ya wapiganaji wake waliokuwa wamekwama kwa zaidi ya miezi miwili katika mji wa Maurip [ ... ]

JESHI LA NATO KUANZA KUFANYA MAZOEZI KUKABILI VITA.
16 May 2022 09:23 - Grace Melleor

Mazoezi makubwa zaidi katika historia ya Baltics ya Muungano wa kijeshi wa NATO yanatarajiwa kuanza baadaye hii leo.

Other Articles

Social Media

Copyright © 2022 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.