Star Tv

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu Prof. Joyce Ndalichako amesema Serikali imedhamiria kutoa fursa kwa vijana nchini ili waweze kuondokana na changamoto ya ajira.

Waziri Ndalichako ameyasema hayo wakati alipoambatana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria walipotembelea mradi wa Kitalu Nyumba (Greenhouse) katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru kwa lengo la kukagua maendeleo ya mafunzo hayo ya kilimo cha kisasa yanayoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu.

“Mheshimiwa Rais amedhamiria kutoa fursa zaidi kwa vijana nchini na serikali anayoiongoza imekuwa ikiwapatia vijana fursa mbalimbali ikiwemo ujuzi na stadi za kazi ili waweze kushiriki kwa ufanisi katika shughuli za uzalishaji mali sambamba na kuongeza fursa za ajira”- Waziri Ndalichako

Amesema kuwa, katika kufanikisha hilo Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu imekuwa ikiratibu Programu ya Taifa ya Kukuza Ujuzi ambayo imelenga kuwezesha nguvu kazi ya Taifa kupata ujuzi na stadi za kazi stahiki ili kumudu ushindani wa soko la ajira na kuwawezesha kujiajiri au kuajiri wenzao.

Aidha, Waziri Ndalichako ametoa wito kwa Viongozi wa Halmashauri kuhakikisha wanatekeleza maagizo ya Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa kwa kuwezesha vijana vitendea kazi kupitia mikopo ya asilimia 10 inayotokana na mapato ya ndani (4% Vijana, 4% Wanawake na 2% Watu wenye Ulemavu ili kuwawezesha vijana hao kufanya kazi au shughuli zenye tija.

Latest News

RAIS WA UKRAINE AAMURU RAIA WOTE KUHAMA MKOA WA DONETSK.
31 Jul 2022 17:17 - Grace Melleor

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ameamuru raia wote ambao bado wanaishi katika maeneo ya mashariki mwa mkoa wa Donetsk [ ... ]

KIFO CHA RAIA WA NIGERIA NCHINI ITALIA CHAZUA HASIRA.
31 Jul 2022 16:58 - Grace Melleor

Kifo cha mhamiaji aliyeshambuliwa mchana kweupe nchini Italia kimezua hasira.

VUTA N’KUVUTE YA MANARA NA KATIBU WA TFF YAIBUKA.
25 Jul 2022 16:37 - Grace Melleor

Katibu Mkuu wa Shrikishi la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Kidao Wilfred amesema amesekitishwa na madai ya yaliyekuwa Af [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2022 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.