Star Tv

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge na Uratibu Balozi, Dkt. Pindi Chana amewataka watumishi wa umma kufanya kazi kwa weledi, ufanisi na kuzingatia taratibu na kanuni zilizopo kwa mujibu wa sheria ili kutoa huduma bora kwa umma.

Dkt. Pindi ametoa kauli hiyo wakati akifungua kikao cha Baraza la Wafanyakazi la Ofisi hiyo na kupokea na kujadili taarifa ya utekelezaji wa bajeti ya Ofisi ya Waziri mkuu kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2021/2022 na makadirio ya bajeti mwaka 2022/ 2023 ambapo amewahimiza kuwa wabunifu katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.

“Baraza hili linazinduliwa kwa mara ya kwanza hivyo kukutana kwenu hapa iwe sehemu muhimu kwenu ya kuibua ubunifu katika mipango yenu na utekelezaji wa shughuli za ofisi kwa kutumia rasilimali zilizopo tuone namna gani tunaweza kubuni mambo mbalimbali katika mipango yetu kuhakikisha umma unapata huduma stahiki na kwa wakati,”- Amesema Dkt. Pindi.

Amesema kwamba lengo la kuanzishwa kwa mabaraza ya wafanyakazi ni kuongeza ufanisi na tija katika sehemu za kazi, waajiri na wafanyakazi kubadilishana mawazo na kubaini mbinu mbalimbali za kukabiliana na changamoto zinazowakabili.

Aidha amewahimiza watumishi hao kuacha kufanya kazi kwa mazoea na kubadilika kifikra katika utendaji wa kazi akisisitiza upendo, bidii ya kazi, uwajibikaji na uadilifu kulingana na dira ya Ofisi hiyo ya kutoa huduma bora kwa umma na kufikia malengo ya serikali.

Wakati huohuo aliitaka Menejimenti kutataua kero za wafanyakazi kwa wakati hatua itakayosaidia kuleta mabadiliko katika maisha yao na ajira kwa ujumla na kuhakikisha wanakuwa na vitendea kazi vya kutosha vitakavyowawezesha kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi na kufanya kazi kwa kujituma.

Latest News

RAIS WA UKRAINE AAMURU RAIA WOTE KUHAMA MKOA WA DONETSK.
31 Jul 2022 17:17 - Grace Melleor

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ameamuru raia wote ambao bado wanaishi katika maeneo ya mashariki mwa mkoa wa Donetsk [ ... ]

KIFO CHA RAIA WA NIGERIA NCHINI ITALIA CHAZUA HASIRA.
31 Jul 2022 16:58 - Grace Melleor

Kifo cha mhamiaji aliyeshambuliwa mchana kweupe nchini Italia kimezua hasira.

VUTA N’KUVUTE YA MANARA NA KATIBU WA TFF YAIBUKA.
25 Jul 2022 16:37 - Grace Melleor

Katibu Mkuu wa Shrikishi la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Kidao Wilfred amesema amesekitishwa na madai ya yaliyekuwa Af [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2022 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.