Star Tv

Mwanamfalme wa Uingereza Harry anataka uamuzi wa Wizara ya Mambo ya ndani ya Uingereza, unaomnyima ulinzi wa polisi wakati anapokuwa Uingereza, uangaliwe upya kupitia mahakama.

Mwanamfalme huyo anasema ameazimia kulipia kazi ya polisi wanaomlinda kwa pesa zake binafsi.

Mwanamfalme Harry -The Duke of Sussex, ambaye anaishi Marekani, anataka kuitembelea nchi yao ya Uingereza na familia yake na anajaribu kuhakikisha kunakuwa na usalama wa mke na watoto wake kwa njia hiyo.

"Uingereza itakuwa nyumbani kwa Mwanamfalme Harry na nchi ambako ana matumaini kwamba mke wake na watoto wako salama".

Ukosefu wa ulinzi wa polisi una hatari kubwa ya kibinafsi," Msemaji wake alisema katika taarifa.

The Duke amesisitiza kuwa ulinzi wa kampuni ya kibinafsi inayomlinda nje ya Uingereza hauwezi kuchukua nafasi ya polisi wa ndani wa Uingereza, ambao wanaweza kupata taarifa za ujasusi na mamlaka muhimu ya kisheria.

Ulinzi wa Uingereza wa Mwanamfalme Harry uliondolewa baada ya kuhamia nchini Marekani na familia yake.

#ChanzoBBC

Latest News

AMPELEKA MKWE MAHAKAMANI KWA KUMZUIA KUOLEWA.
17 May 2022 06:34 - Grace Melleor

Binti aliyefahamika kwa jila la Halima Yunusa Ibrahim amempeleka babamkwe wake latika Mahakama ya Kiislamu Islamic (Shar [ ... ]

WANAJESHI WA UKRAINE WALIOZINGIRWA WALIOKOLEWA.
17 May 2022 05:50 - Grace Melleor

Ukraine imethibitisha kwamba mamia ya wapiganaji wake waliokuwa wamekwama kwa zaidi ya miezi miwili katika mji wa Maurip [ ... ]

JESHI LA NATO KUANZA KUFANYA MAZOEZI KUKABILI VITA.
16 May 2022 09:23 - Grace Melleor

Mazoezi makubwa zaidi katika historia ya Baltics ya Muungano wa kijeshi wa NATO yanatarajiwa kuanza baadaye hii leo.

Other Articles

Social Media

Copyright © 2022 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.