Star Tv

Mawimbi ya Tsunami yaliyosababishwa na mlipuko mkubwa wa volkano chini ya maji yameikumba nchi ya Pasifiki ya Tonga.

Picha za mitandao ya kijamii zilionyesha maji yakipita kwa kasi eneo la kanisani na nyumba kadhaa, na walioshuhudia walisema majivu yalikuwa yakianguka kwenye mji mkuu, Nuku'alofa.

Tahadhari ya tsunami iliyotolewa iliwafanya wakazi kukimbilia maeneo ya miinuko

Mlipuko wa volcano ya Hunga Tonga-Hunga Haʻapai ulisikika Pasifiki ya Kusini, ikiripotiwa hadi New Zealand na Australia.

Mji mkuu wa Tonga uko kilomita 65 Kaskazini ya eneo lililokumwa na mlipuko wa volcano, kwenye kisiwa kikuu cha Tongatapu nchini humo.

 

Mabomba ya gesi, moshi na majivu yanayomiminika kutoka kwenye volcano yalifikia kilomita 20 angani, Huduma za Jiolojia za Tonga zilisema.

Wenyeji walisema mlipuko huo ulisikika kama ngurumo ya radi, ikifuatiwa na anga giza huku mawingu ya volkeno yakianza "kunyesha majivu na kokoto ndogo".

Maeneo mengi ya Tonga yanakabiliwa na uhaba wa umeme, huku huduma za simu na intaneti zikikatizwa, Kumaanisha mawasiliano yalikatizwa. Lakini video kwenye mitandao ya kijamii zilionyesha msongamano mkubwa wa magari huku watu wakijaribu kukimbilia maeneo ya juu kwa gari.

#ChanzoBBC

Latest News

AMPELEKA MKWE MAHAKAMANI KWA KUMZUIA KUOLEWA.
17 May 2022 06:34 - Grace Melleor

Binti aliyefahamika kwa jila la Halima Yunusa Ibrahim amempeleka babamkwe wake latika Mahakama ya Kiislamu Islamic (Shar [ ... ]

WANAJESHI WA UKRAINE WALIOZINGIRWA WALIOKOLEWA.
17 May 2022 05:50 - Grace Melleor

Ukraine imethibitisha kwamba mamia ya wapiganaji wake waliokuwa wamekwama kwa zaidi ya miezi miwili katika mji wa Maurip [ ... ]

JESHI LA NATO KUANZA KUFANYA MAZOEZI KUKABILI VITA.
16 May 2022 09:23 - Grace Melleor

Mazoezi makubwa zaidi katika historia ya Baltics ya Muungano wa kijeshi wa NATO yanatarajiwa kuanza baadaye hii leo.

Other Articles

Social Media

Copyright © 2022 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.