Bomu limelipuka katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu huku kukiwa na ripoti kwamba watu kadhaa wamepoteza maisha kutokana na mlipuko wa bomu hilo.
Mlipuko huo ulitokea kwenye barabara ya eneo la kuingilia kambi ya Jeshi la wana anga la Somalia ambayo iko karibu na uwanja wa ndege wa kimataifa.
Ingawa bado haijafahamika ni nani aliyehusika na shambulio hilo, kundi la wanamgambo wa Kiislamu la Al Shabab mara kwa mara hutekeleza mashambulizi ya kujitoa mhanga.
#ChanzoBBC