Star Tv

Gari la waandishi wa habari Mkoa wa Mwanza lililokuwa kwenye ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza limepata ajali eneo la Busega ambalo lilikuwa linaelekea Ukerewe kupitia Bunda.

Mwenyekiti wa Mwanza Press Club Edwin Soko ametoa taarifa hiyo ambapo amebainisha kuwa "Nimeongea na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel amethibitisha kupokea taarifa za watu watano waliokuwa kwenye gari hilo lililobeba waandishi kufariki"- Soko.

Gari hilo hilo limepata ajali baada ya kugongana na gari ya abiria aina ya Toyota Hiace katika eneo la Nyamikoma wilayani Busega mkoani Mwanza.
Kwa sasa Mkuu wa Mkoa ameelekea eneo la tukio ilipotokea ajali hiyo, Bado idadi kamili ya watu waliofariki na majeruhi haijafahamika lakini kunahofiwa kuna zaidi ya watu wanne wameaga dunia.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyo, Blasius Chatanda amesema yupo katika hospitali ambako majeruhi walikopelekwa akiahidi kuwa atatoa taarifa baadaye.

Latest News

RAIS WA UKRAINE AAMURU RAIA WOTE KUHAMA MKOA WA DONETSK.
31 Jul 2022 17:17 - Grace Melleor

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ameamuru raia wote ambao bado wanaishi katika maeneo ya mashariki mwa mkoa wa Donetsk [ ... ]

KIFO CHA RAIA WA NIGERIA NCHINI ITALIA CHAZUA HASIRA.
31 Jul 2022 16:58 - Grace Melleor

Kifo cha mhamiaji aliyeshambuliwa mchana kweupe nchini Italia kimezua hasira.

VUTA N’KUVUTE YA MANARA NA KATIBU WA TFF YAIBUKA.
25 Jul 2022 16:37 - Grace Melleor

Katibu Mkuu wa Shrikishi la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Kidao Wilfred amesema amesekitishwa na madai ya yaliyekuwa Af [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2022 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.