Star Tv

Rais Samia Suluhu Hassana amesema amewapa kazi mpya aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi na aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi.

Rais Samia ameyasema hayo leo Jumatatu Januari 10, 2022 muda mfupi baada ya kuwaapisha mawaziri na naibu mawaziri, makatibu na naibu makatibu wakuu wa wizara mbalimbali Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma.

Rais Samia amesema "Nina kaka zangu wawili William Lukuvi na Profesa Palamagamba Kabudi, wana umri kama wangu. Lukuvi ana kazi maalum na mtaisikia hivi karibuni, Profesa Kabudi amefanya kazi nzuri sana katika majadiliano ya ubia kwenye mashirika ya serikali. Kaka zangu hawa (Profesa Kabudi na William Lukuvi) bado nina kazi nao, nimewavuta Ikulu. Acheni maneno maneno wamefanya kazi nzuri, na wamelitumikia Taifa kwa uadilifu na uaminifu mkubwa, waacheni waje kwangu tumalize nao pamoja” amesema Rais Samia.

Rais Samia ameisifia kazi nzuri aliofanya Kabudi kuhusu mazungumzo ya serikali na mashirika. "Ila kazi yake kwa sababu haiko kwenye muundo haitangazwi wala nini lakini atasimamia hiyo kazi ..mashirika yote kazi zote zitakazoingia ubi ana serikali,Kabudi ataongoza hiyo team".Kakangu Lukuvi yeye ana kazi na mimi.Mtaisikia baadaye lakini namvuta Ikulu kazi yetu ni kuwasimamia nyinyi".

Rais Samia amewaapisha Mawazir, Manabu Waziri pamoja Makatibu na manaibu katibu wakuu wa wizara mbalimbali. Hafla iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson.

 

Latest News

MATETEMEKO MAWILI YA ARDHI YAUA WATU 22 AFGHANISTAN.
18 Jan 2022 09:36 - Grace Melleor

Takriban watu 22 wafariki kufikia sasa baada ya matetemeko ya ardhi ya mfululizo kukumba magharibi mwa Afghanistan siku  [ ... ]

WAZIRI MKUU AWATAKA MABALOZI KUVUTIA WAWEKEZAJI.
17 Jan 2022 16:24 - Grace Melleor

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania katika mataifa mbalimbali watoe msukumo Katika u [ ... ]

RAIS WA MALI ALIYEPENDULIWA MADARAKANI AFARIKI.
17 Jan 2022 06:53 - Grace Melleor

Rais wa Mali aliyeondolewa madarakani Ibrahim Boubacr Keita amefariki akiwa na umri wa miaka 76, familia yake na rafiki  [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2022 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.