Star Tv

Takriban watu 164 wamekufa nchini Kazakhstan wakati wa maandamano ya kupinga serikali, kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari zilizowanukuu maafisa wa afya.

Iwapo itathibitishwa itaashiria ongezeko kubwa kutoka kwa idadi ya awali ya vifo 44.

Takriban watu 6,000 wamekamatwa, ikiwa ni pamoja na "idadi kubwa ya raia wa kigeni", ofisi ya rais ya Kazakhstan ilisema Jumapili.

Maandamano hayo, yaliyochochewa na kupanda kwa bei ya mafuta, yaligeuka kuwa ghasia kubwa huku yakienea nchini kote.

Walianza tarehe 2 Januari na walikua wakionesha kutoridhika na serikali na Rais wa zamani Nursultan Nazarbayev, ambaye aliongoza Kazakhstan kwa miongo mitatu, bado anafikiriwa kuwa na ushawishi mkubwa.

Wiki iliyopita, wanajeshi kutoka nchi zikiwemo Urusi walitumwa Kazakhstan kusaidia kurejesha utulivu.

Taarifa ya Rrais imeongeza kuwa hali imetulia, huku wanajeshi wakiendelea na operesheni za "usafishaji" na kulinda "vifaa vya kimkakati".

Aidha hali ya hatari na amri ya kutotoka nje kwa nchi nzima bado imesalia.

Latest News

RAIS WA UKRAINE AAMURU RAIA WOTE KUHAMA MKOA WA DONETSK.
31 Jul 2022 17:17 - Grace Melleor

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ameamuru raia wote ambao bado wanaishi katika maeneo ya mashariki mwa mkoa wa Donetsk [ ... ]

KIFO CHA RAIA WA NIGERIA NCHINI ITALIA CHAZUA HASIRA.
31 Jul 2022 16:58 - Grace Melleor

Kifo cha mhamiaji aliyeshambuliwa mchana kweupe nchini Italia kimezua hasira.

VUTA N’KUVUTE YA MANARA NA KATIBU WA TFF YAIBUKA.
25 Jul 2022 16:37 - Grace Melleor

Katibu Mkuu wa Shrikishi la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Kidao Wilfred amesema amesekitishwa na madai ya yaliyekuwa Af [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2022 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.