Star Tv

Rais Joe Biden wa Marekani atafanya mazungumzo kwa njia ya simu leo na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin katika juhudi za kutuliza mvutano kuhusu hatua ya Urusi kupeleka vikosi vyake kwenye mpaka na Ukraine.

Yatakuwa mazungumzo ya pili ya simu katika chini ya mwezi mmoja baina ya viongozi hao, huku Biden mapema Desemba akimuonya Putin kuhusu madhara makubwa kama wanajeshi wa Urusi wataivamia Ukraine.

Mazungumzo ya leo kati ya Biden na Putin yatafanyika wakati Marekani na washirika wake wa magharibi wameshuhudia Urusi ikiendelea kulundika mamia kwa maelfu ya wanajeshi wake karibu na mpaka na Ukraine hali inayozidisha wasiwasi kuwa Kremlin ina mipango ya kuivamia nchi hiyo.

Katika mkutano wa leo ambao uliombwa na Urusi, Biden anatarajiwa kumweleza kwa mara nyingine na bila kificho Putin kwamba Washington inasimama imara na kwa mshikamano na washirika wake wa magharibi lakini itakuwa tayari kufanya mazungumzo na Urusi chini ya diplomasia ya kuheshimiana.

Latest News

MATETEMEKO MAWILI YA ARDHI YAUA WATU 22 AFGHANISTAN.
18 Jan 2022 09:36 - Grace Melleor

Takriban watu 22 wafariki kufikia sasa baada ya matetemeko ya ardhi ya mfululizo kukumba magharibi mwa Afghanistan siku  [ ... ]

WAZIRI MKUU AWATAKA MABALOZI KUVUTIA WAWEKEZAJI.
17 Jan 2022 16:24 - Grace Melleor

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania katika mataifa mbalimbali watoe msukumo Katika u [ ... ]

RAIS WA MALI ALIYEPENDULIWA MADARAKANI AFARIKI.
17 Jan 2022 06:53 - Grace Melleor

Rais wa Mali aliyeondolewa madarakani Ibrahim Boubacr Keita amefariki akiwa na umri wa miaka 76, familia yake na rafiki  [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2022 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.