Star Tv

Mwili wa Hayati Askofu Mkuu Desmond Tutu umewasili katika Kanisa Kuu la Mtakatifu George mjini Cape Town ambapo utalala kwa siku mbili kwa heshima ya kitaifa.

Tutu, mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel ambaye alisaidia kukomesha ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini, alifariki Jumapili akiwa na umri wa miaka 90.

Mazishi yake rasmi ya kiserikali yatafanyika tarehe 1 Januari baada ya kipindi cha kulazwa, kuruhusu waombolezaji kuupita mwili wake na kuuaga kwa mara ya mwisho.

Muda wa kulazwa katika kanisa hilo ulilazimika kuongezwa hadi siku mbili, "kwa kuhofia kunaweza kutokea mkanyagano," kasisi wa eneo hilo aliliambia shirika la habari la AFP.

Umma utaweza kutoa heshima zao kwa kiongozi huyo wa kidini anayeheshimika sana, nguzo muhimu katika mapambano ya kukomesha mfumo wa ubaguzi wa rangi uliotekelezwa na serikali ya wazungu wachache dhidi ya weusi walio wengi nchini Afrika Kusini kuanzia 1948 hadi 1991.

Ibada za ukumbusho zitafanyika kote Afrika Kusini huku usiku wa karibu wa ukumbusho na marafiki zake wa karibu utafanyika baadaye.

Baada ya mazishi ya Jumamosi, mabaki ya Tutu yatachomwa na majivu yake kuwekwa katika kanisa kuu, ambapo alihubiri kwa miaka mingi.

#ChanzoBBC

 

Latest News

MATETEMEKO MAWILI YA ARDHI YAUA WATU 22 AFGHANISTAN.
18 Jan 2022 09:36 - Grace Melleor

Takriban watu 22 wafariki kufikia sasa baada ya matetemeko ya ardhi ya mfululizo kukumba magharibi mwa Afghanistan siku  [ ... ]

WAZIRI MKUU AWATAKA MABALOZI KUVUTIA WAWEKEZAJI.
17 Jan 2022 16:24 - Grace Melleor

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania katika mataifa mbalimbali watoe msukumo Katika u [ ... ]

RAIS WA MALI ALIYEPENDULIWA MADARAKANI AFARIKI.
17 Jan 2022 06:53 - Grace Melleor

Rais wa Mali aliyeondolewa madarakani Ibrahim Boubacr Keita amefariki akiwa na umri wa miaka 76, familia yake na rafiki  [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2022 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.