Star Tv

Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Kamishina Msaidizi wa Polisi ACP. Justine Masejo leo Desemba 28.2021 ametoa taarifa juu ya tukio la mauaji ya marehemu Ruth Mmasi lililotokea mwishoni mwa wiki iliyopita mwaka huu 2021 huko maeneo ya Njiro katika halmashauri ya jiji la Arusha.

ACP. Masejo amesema Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo na linamshikilia mtu mmoja kwa mahaojiano ya kina juu ya tukio hilo ambalo lilipelekea umauti wa marehemu Ruth Mmasi.

Kamanda masejo ameendelea kusema kuwa mtuhumiwa ambae anatuhumiwa anaendelea kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi na kupelekea kupata baadhi ya vielelezo kuhusiana na tukio hilo.

Ameeleza kuwa Chanzo cha tukio hilo bado kinachunguzwa na amewaomba wananchi, ndugu na jamaa kuwa wavumilivu wakati Polisi wakiendelea na uchunguzi wa kina kuhusiana na tuko hilo.

Ametoa wito kwa viongozi wa dini na makundi mbalimbali ya kijamii na kimila kuendelea kuelimisha wananchi kutojichukulia sheria mkononi, kitendo ambacho ni kinyume na sheria za nchi yetu.

Latest News

RAIS WA UKRAINE AAMURU RAIA WOTE KUHAMA MKOA WA DONETSK.
31 Jul 2022 17:17 - Grace Melleor

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ameamuru raia wote ambao bado wanaishi katika maeneo ya mashariki mwa mkoa wa Donetsk [ ... ]

KIFO CHA RAIA WA NIGERIA NCHINI ITALIA CHAZUA HASIRA.
31 Jul 2022 16:58 - Grace Melleor

Kifo cha mhamiaji aliyeshambuliwa mchana kweupe nchini Italia kimezua hasira.

VUTA N’KUVUTE YA MANARA NA KATIBU WA TFF YAIBUKA.
25 Jul 2022 16:37 - Grace Melleor

Katibu Mkuu wa Shrikishi la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Kidao Wilfred amesema amesekitishwa na madai ya yaliyekuwa Af [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2022 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.