Vikwazo vikali vya kuzuia kusambaa kwa virusi vya Corona vitaanza kutumika kuanzia leo Jumanne katika majimbo kadhaa ya Ujerumani katika wakati inakabiliwa na wimbi la tano la maambukizo ya ugonjwa wa Covid-19.
Wakazi katika majimbo ya Bavaria, Berlin, Hesse, North Rhine Westphalia, Saarland, Saxony, Schleswig Holstein na Thuringia watakabiliwa na vikwazo hivyo vipya.
Vikwazo hivyo pia vitaanza kutumika katika majimbo mengine huku maafisa wa afya wakijaribu kuzuia kuenea kwa aina mpya ya kirusi cha Omicron.
Viongozi wa majimbo na wale wa serikali kuu walikubaliana kuweka vikwazo zaidi kuanzia Disemba 28, wakati kila jimbo likitwikwa jukumu la kutekeleza vikwazo hivyo.
Maafisa wana wasiwasi juu ya kuongezeka kwa maambukizo mapya kutokana na kirusi cha Omicron, ambacho sasa kimeenea katika majimbo yote 16 ya Ujerumani.
#ChanzoDW