Star Tv

Waziri Mkuu wa Somalia amesema anaviamuru vikosi vyote vya usalama kuchukua amri moja kwa moja kutoka kwake na sio kutoka kwa Rais.

Kauli hiyo ya Roble imeonyesha kuzua uwezekano wa kuongezeka kwa mvutano kati yake na rais Mohammed Abdullahi Mohammed al maarufu Farmajo.

Mapema leo, Roble alimshtumu Raisi wake kwa kupanga jaribio la mapinduzi.

Katika taarifa iliyochapishwa katika mtandao wa Facebook wa shirika la habari la SONNA nchini humo, Roble amesema anataka kuwaambia watu wa Somalia kwamba hatua zilizochukuliwa na Farmajo ni jaribio wazi la mapinduzi dhidi ya serikali na katiba ya kitaifa.

Mvutano huo unaonekana kwa kiasi kikubwa kama juhudi za kuitatiza serikali kukabiliana na makundi ya waasi na umeifanya Marekani kutoa wito wa utulivu.

Latest News

RAIS WA UKRAINE AAMURU RAIA WOTE KUHAMA MKOA WA DONETSK.
31 Jul 2022 17:17 - Grace Melleor

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ameamuru raia wote ambao bado wanaishi katika maeneo ya mashariki mwa mkoa wa Donetsk [ ... ]

KIFO CHA RAIA WA NIGERIA NCHINI ITALIA CHAZUA HASIRA.
31 Jul 2022 16:58 - Grace Melleor

Kifo cha mhamiaji aliyeshambuliwa mchana kweupe nchini Italia kimezua hasira.

VUTA N’KUVUTE YA MANARA NA KATIBU WA TFF YAIBUKA.
25 Jul 2022 16:37 - Grace Melleor

Katibu Mkuu wa Shrikishi la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Kidao Wilfred amesema amesekitishwa na madai ya yaliyekuwa Af [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2022 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.