Star Tv

Marekani imemaliza vikwazo vilivyowekwa dhidi ya Burundi miaka sita iliyopita, ikitoa mfano wa mageuzi nchini humo.

Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ilibainisha kuwa Rais Joe Biden alibatilisha amri iliyoidhinisha vikwazo hivyo.

Ilikubali uchaguzi wa mwaka jana ambao ulimleta Rais Évariste Ndayishimiye na mageuzi ambayo amefuata "katika sekta nyingi".

"Tunatambua hatua zilizoafikiwa na Rais Ndayishimiye katika kushughulikia biashara haramu ya binadamu, mageuzi ya kiuchumi, na kupambana na rushwa na kuhimiza maendeleo endelevu," - Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken alisema.

Naibu Katibu wa Hazina ya Marekani, Wally Adeyemo, alisema katika taarifa tofauti kwamba Marekani itaendelea kuishinikiza Burundi "kuboresha hali ya haki za binadamu nchini humo na kuwawajibisha wale wanaohusika na ukiukaji na unyanyasaji".

Marekani na Umoja wa Mataifa ziliweka vikwazo dhidi ya Burundi mwaka 2015 ikiwa ni pamoja na vikwazo vya visa na kufungia mali za maafisa wakuu serikalini.

Zaidi ya watu 1,000 waliuawa na mamia ya maelfu wengine walikimbia nchi katika ghasia zilizofuata.

Aidha Rais Ndayishimiye kupitia ujumbe wa twitter amekaribisha hatua ya Marekani kuiondolea nchi yake vikwazo.

#ChanzoBBCSwahili

Latest News

SHAMBULIO LA KUJITOA MHANGA LAUA WATU NANE SOMALIA.
25 Nov 2021 10:26 - Grace Melleor

Polisi nchini Somalia wamethibitisha vifo vya raia katika bomu lililotegwa ndani ya gari katika mji mkuu Mogadishu, tele [ ... ]

WAZIRI MKUU SWEDEN AJIUZULU SAA CHACHE BAADA YA KUTEULIWA.
25 Nov 2021 09:01 - Grace Melleor

Waziri Mkuu wa kwanza mwanamke kuwahi kushikilia wadhifa huo nchini Sweden amejiuzulu saa chache mara baada ya kuteuliwa [ ... ]

MTOTO WA GADDAFI AZUIWA KUGOMBEA URAIS LIBYA.
25 Nov 2021 07:13 - Grace Melleor

Mtoto wa aliyekuwa kiongozi wa Libya hayati Muammar Gaddafi ameenguliwa katika kinyang’anyiro cha kuwania uchaguzi wa  [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.