Star Tv

Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango amewahakikishia watanzania wanaoishi nje ya Tanzania kwamba serikali inatambua mchango wao katika ujenzi wa taifa na hivyo itaendelea kutatua changamoto zote zinazokwamisha wao kuwekeza nchini Tanzania.

Makamu wa Rais amesema kuanzishwa na idara maalum inayoshughulikia masuala ya watanzania wanaoishi nje ya Tanzania katika Wizara ya Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki ni ishara thabiti ya kutambua kwa vitendo mchango wa diaspora katika taifa.

Dkt. Philip Mpango amebainisha hayo leo Novemba 16,2021 akiwa nchini Singapore ambapo amekutana na kufanya mazungumzo na Watanzania waishio Singapore.

Amewakaribisha watanzania hao kuwekeza nchini Tanzania huku akiwakikishia kwamba serikali imeweka mkazo katika kuvutia uwekezaji pamoja na kuboresha sekta ya biashara.

Kwa Upande wao watanzania wanaoishi nchini Singapore wamepongeza jitihada zinazochukuliwa na Tanzania katika kutafuta muafaka wa hadhi maalum kwaajili yao ili kuwapa nafasi ya kuwekeza kikamilifu nchini.

Wameiomba serikali kuendelea kutatua changamoto hasa katika masuala ya kodi pamoja na vibali vya kazi kwa wataalam mbalimbali wanaolenga kuwaleta kutoa huduma Tanzania.

Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mbarouk Mbarouk amesema Wizara inaendelea kuchukua hatua mbalimbali katika kutafuta muafaka wa kuwapa hadhi maalum diaspora na kuwakaribisha kurejesha ujuzi walioupata nchi za nje katika kujenga uchumi wa Tanzania.

Katika hatua nyingine Makamu wa Rais amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Heshima wa Tanzania Nchini Singapore Teo Sieng Seng, Ambapo amempongeza balozi huyo kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuitangaza Tanzania huku akimueleza kwamba Tanzania ni nchi salama na yenye utulivu na Amani iliyoweka mkazo katika kuvutia wawekezaji hivyo kumuomba kuendelea kutoa mchango wake katika kukuza biashara na kuongeza watalii na wawekezaji hapa nchini.

Latest News

SHAMBULIO LA KUJITOA MHANGA LAUA WATU NANE SOMALIA.
25 Nov 2021 10:26 - Grace Melleor

Polisi nchini Somalia wamethibitisha vifo vya raia katika bomu lililotegwa ndani ya gari katika mji mkuu Mogadishu, tele [ ... ]

WAZIRI MKUU SWEDEN AJIUZULU SAA CHACHE BAADA YA KUTEULIWA.
25 Nov 2021 09:01 - Grace Melleor

Waziri Mkuu wa kwanza mwanamke kuwahi kushikilia wadhifa huo nchini Sweden amejiuzulu saa chache mara baada ya kuteuliwa [ ... ]

MTOTO WA GADDAFI AZUIWA KUGOMBEA URAIS LIBYA.
25 Nov 2021 07:13 - Grace Melleor

Mtoto wa aliyekuwa kiongozi wa Libya hayati Muammar Gaddafi ameenguliwa katika kinyang’anyiro cha kuwania uchaguzi wa  [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.